MALI-MNLA-AU-Mazungumzo

Mali: Mohamed Ould Abdel Azizi, mwenyekiti wa AU ziarani Kidal

Mohamed Ould Abdel Aziz, lrais wa Mauritania akiwa pia mwenyekiti wa Umoja wa Mataifa, alipowasili katika mji wa Kidal, Ijumaa Me 23 mwaka 2014.
Mohamed Ould Abdel Aziz, lrais wa Mauritania akiwa pia mwenyekiti wa Umoja wa Mataifa, alipowasili katika mji wa Kidal, Ijumaa Me 23 mwaka 2014. DR / UN

Duru za kidiplomasia kutoka Umoja wa Mataifa ziliyotajwa na shirika la habari la Ufaransa AFP zimefahamisha kwamba rais wa Mauritania akiwa pia mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Mohamed Ould Abdel Aziz, “amewasili katika mji wa Kidal unaoshikiliwa na waasi wa MNLA.

Matangazo ya kibiashara

Lengo la ziara hio ya kushitukiza ni kujaribu kutafuta suluhu la mgogoro unaoendelea”. Rais huyo wa Mauritania ameshirikiana katika ziara hio na mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali, Bert Koenders. Ziara hio ya rais Mohamed inakuja siku moja baada ya kukutana kwa mazungumzo na rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita mjini Bamako.

Majeshi ya Mali yalitimuliwa hivi karibuni na makundi ya waasi kutoka jamii ya Tuareg katika mji wa Kidal nchini Mali. Hali hio inatiya wasiwasi jumuiya ya kimataifa, na mataifa mbalimbali yameanza kushawishi pande mbili kuketi kwenye meza ya mazungumzo.

Rais huyo amesafiri katika mji wa Gao akitumia helikopta nyeupe ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali Minusma, huku ikilindwa na helikopta ya kijeshi ya Ufaransa. Ndege hizo zilitua katika kambi ya wanajeshi wa vikosi vya Ufaransa na Umoja wa Mataifa.

Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Afrika amepanga kukutana kwa mazungumzo na viongozi wa makundi matatu ya waasi MNLA,HCUA na kundi la waasi la MAA. Kukutana na viongozi wa makundi hayo, Mohamed Oul abdel Aziz atajaribu kuwaeleza umuhimu wa kuketi kwenye meza ya mazungumzo na serikali, duru kutoka ikulu ya Mauritania zimethibitisha.

Kwa mujibu wa msemaji wa MNLA, Mossa Ag Attaher, rais Aziz amekuja kuokoa mchakato wa amani uliyokua umedororora kutokana na serikali ambayo haikua na utashi wa kupatia ufumbuzi baadhi ya madai yao.