MALI-MNLA-Siasa-Dilpomasia

Mali: serikali yatakiwa kuketi pamoja na waasi

Waandamanaji wakiwa mbele ya ubalozi wa Ufaransa, huku wakilani kusdhibitiwa na waasi wa MNLA kwa mji wa Kidal.
Waandamanaji wakiwa mbele ya ubalozi wa Ufaransa, huku wakilani kusdhibitiwa na waasi wa MNLA kwa mji wa Kidal. AFP PHOTO / HABIBOU KOUYATE

Viongozi wa Mali wameanza kushinikizwa na jumuiya ya kimataifa kufufua mazungumzo na waasi kutoka jamii ya Tuareg, baada ya kupoteza mamlaka katika miji ya Kidal na Meneka, Umoja wa Mataifa umethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Ufaransa ambayo ina wanajeshi 1700 nchini Mali, imeimarisha ngome zake kaskazini mwa taifa hilo, huku ikitupilia mbali uingiliaji kati katika masuala ya usalama wa ndani wa Mali. Hata hivo Umoja wa Mataifa umebaini kwamba kikosi chake cha wanajeshi 12.600 Mali hakiko Mali kwa ajili ya mapigano, bali kusaidia kupatikana suluhu mzozo wa kisiasa.

Kauli hio ya Umoja wa Mataifa inakwenda sambamba na kauli ya mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz, akiwa pia mmoja wa wanaharakati muhimu dhidi ya ugaidi katika eneo la Sahel, ambae yuko ziarani nchini Mali.

Rais wa Mauritania, Mohamed Abdel Aziz, akiwa mwenyekilti wa Umoja wa Afrika.
Rais wa Mauritania, Mohamed Abdel Aziz, akiwa mwenyekilti wa Umoja wa Afrika. (Photo : M. Rivière / RFI)

Hayo yakijiri, hapo jana alhamisi raia waliandamana katika miji ya Bamako, Gao na Tombouctou wa kichukulia kauli ya viongozi wa Mali dhidi ya vikosi vya wanajeshi wa Ufaransa “Serval” na Umoja wa Mataifa (Minusma) kwa kutojua wajibu wao wa kuwalindia usalama raia.

Viongozi wa Mali wanasadikiwa kuwa walipendelea vikosi hivyo kushirikiana na jeshi lake kwa kuwatimua waasi, kama ilivyokua nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya kundi la waasi la M23.