DRCONGO

Mahakama ya ICC yamhukumu Katanga miaka 12 jela kwa uhalifu wa kivita

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, imemhukumu kifungo cha miaka 12 jela aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi la FRPI , Germain Katanga al maarufu Simba kufuatia mauaji yaliyotekelezwa na kundi lake mwaka 2003 kijijini Bogoro nchini DRC. 

Germain Katanga,kiongozi wa zamani wa kundi la uasi la  FRPI nchini DRC
Germain Katanga,kiongozi wa zamani wa kundi la uasi la FRPI nchini DRC AFP PHOTO / ANP / POOL
Matangazo ya kibiashara

Jaji kiongozi katika kesi hiyo,Bruno Cotte amesema kuwa mahakama imemkuta na hataia ya kushiriki kupanga njama na kutekeleza mauaji dhidi ya raia kwenye mji wa Bogoro.

Hata hivyo Jaji Cotte amesema kuwa miaka saba ambayo Katanga ametumia akiwa kizuizini itaondolewa kwenye hukumu hiyo iliyotollewa jana Ijumaa.

 

Katanga mwenye umri wa miaka 36, alikamatwa mwezi Machi kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwemo mauaji na unyang'anyi, na kwa kushiriki katika mashambulizi ya kijiji cha Bogoro Mashariki mwa DRC mnamo Februari 24, 2003.

Majaji wamegundua kuwa aliwapa silaha wapiganaji wa kundi la Patriotic Resistance Forces (FRPI) mjini Ituri ambao walifanya mauaji ya halaiki kijijini hapo na kuua watu zaidi ya 200.