NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Nigeria: wasichana waliotekwa nyara wajulikana waliko

Jenerali Chris Olukolade,msemaji wa wizara ya ulinzi ya Nigeria.
Jenerali Chris Olukolade,msemaji wa wizara ya ulinzi ya Nigeria. AFP PHOTO/PIUS UTOMI EKPEI

Jeshi la Nigeria linasema linafahamu ni wapi waliko zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara na kundi la kigaidi la Boko Haram , zaidi ya mwezi mmoja uliopita, bila hata hivo kutaja waliko.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa majeshi nchini humo Alex Badeh amewaambia wanahabari jijini Abuja kuwa licha ya kufahamu waliko wasichana hao, hawawezi kutumia nguvu kuwaondoa mikononi mwa Boko Haram.

Bade amesisitiza kuwa jeshi liachwe lifanye kazi yake, na kuongeza kuwa ni habari njema kwa wasichana na wazazi wao.

Aboubakar Shekau, kiongozi wa kundi la Boko Haram,katika mkanda uliyorushwa na kundi hilo Mei 12 mwaka 2014.
Aboubakar Shekau, kiongozi wa kundi la Boko Haram,katika mkanda uliyorushwa na kundi hilo Mei 12 mwaka 2014. AFP PHOTO / BOKO HARAM

Kutekwa nyara kwa wanafunzi 276 wakiwemo 223 ambao bado wanashikiliwa na kundi la Boko Haramu tangu katikati ya mwezi wa Aprili walipoondolewa katika shule lao katika eneo la Chibok (kaskazini mashariki), kulizuwa hisia mbalimbali na kupelekea mataifa mbalimbali duniani kutoa mchango wao ili kuhakikisha kuwa wasichana hao wamepatikana.

Serikali ya Nigeria imekuwa ikipata shinikizo kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo na kwingineko duniani, kuhakikisha kuwa wasichana hao wanaachiliwa huru.

Serikali ya Nigeria imesema haiwezi kubadilishana wafungwa na kundi hilo na wasichana hao.

Waandamanaji , katika mji wa Lagos, nchini Nigeria, le Mei 14 mwaka 2014.
Waandamanaji , katika mji wa Lagos, nchini Nigeria, le Mei 14 mwaka 2014. REUTERS/Akintunde Akinleye

Hata hivo licha ya kuwa serikali ya Nigeria ililaumiwa kuhusu kushindwa kuwajibika ili wasichana hao wapatikane, ilikubali hivi karibuni mchango wa mataifa ya magharibi kushiriki katika jitihada za kuwatafuta wanafunzi hao waliyotekwa nyara na Boko Haram.

Marekani, Uingereza, Ufaransa na hivi karibuni Israel waliwatuma wataalamu wao kwa kusaidia nchi ya Nigeria katika jitihada hizo. China ambayo raia wake kumi walitekwa nyara na kundi la Boko Haram katika jimbo linaopakana na Cameroon, ilipendekeza mchango wake.