Mali: waziri mpya wa ulinzi ateuliwa
Imechapishwa: Imehaririwa:
Wiki moja baada ya jeshi la Mali kupata pigo kubwa katika mji wa Kidal baada ya mapigano kati ya jeshi na waasi kutoka jamii ya Tuareg, waziri wa Mali wa ulinzi, Soumeylou Boubèye Maïga, amejiuzulu kwenye wadhifa huo na Ba N'Dao, afisa wa ngazi ya juu jeshini aliestaafu ameteuliwa kuchikilia wadhifa huo.
Soumeylou Boubèye Maïga, ambae aliwahi kua mkuu wa idara ya Intelejensia , pia waziri wa mambo ya kigeni na baadae waziri wa ulinzi, ni mtu muhimu alieleta mabadiliko katika siasa ya Mali.
Soumeylou Boubèye Maïga, anachukuliwa kama jasiri, na mshirika wa karibu wa rais Ibrahim Boubacar Keïta, ambae alimteua kwenye wadhifa huo muhimu baada ya kuchukua mamlaka ya nchi.
Soumeylou Boubèye Maïga, alikua akisimamia kwa ushirikiano na Umoja wa Ulaya (EU) shughuli za kuunda upya jeshi la Mali, ambalo lilikua lilipoteza imani kwa wananchi wake mwanzoni mwa mwaka 2012 kutokana na mashambulizi ya waasi wa Tuareg, ambao walitimuliwa baada ya operesheni ya vikosi vya kimataifa iliyoanzishwa na Ufaransa mwezi wa Januari mwaka 2013.
Afisa huyo wa ngazi ya juu jeshini, alihusika na kuwakamata wanajeshi walipaka tope jeshi la Mali, akiwemo Amadou Haya Sanogo na washirika wake wengi, ambao walihusika katika jaribio la mapinduzi la Machi 2012, ambalo lilisababisha Mali inaingia katika machafuko.
Hapo Jumanne jioni, ikulu ya Mali ilitoa tangazo kuhusu kuteuliwa kwa Ba N'Dao kwenye wadhifa wa waziri wa ulinzi, uliyokua ukishikiliwa na Soumeylou Boubèye Maïga.
Kwa mujibu wa watu waliyo karibu na kiongozi huyo, Maïga amechukua uamzi wa kujiuzulu kwa hiari yake, baada ya kusikia kwamba kuna mabadiliko ambayo yanatazamiwa kufanywa kwenye ngazi ya jeshi kutokana na kushindwa kwa jeshi dhidi ya majundi ya kislamu kaskazini mwa Mali.