MISRI-Uchaguzi

Abdel Fattah al-Sisi apata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa urais Misri

Aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Misri, Abdel Fatah al-Sisi ambaye ameshinda uchaguzi wa mwaka huu.
Aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Misri, Abdel Fatah al-Sisi ambaye ameshinda uchaguzi wa mwaka huu. Reuters

Kiongozi wa zamani wa jeshi nchini Misri, Abdel Fattah al-Sisi amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa urais uliofanyika wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Matokeo kutoka tume ya Uchaguzi yanaonesha kuwa Al Sisi amepata asilimia 96 ya kura zote zilizopigwa na tayari mpinzani wake wa pekee Hamdeen Sabbahi, aliyepata asilimia 4 amekiri kushindwa.

Wafuasi wa Al sisi wanasherekea katika mitaaa ya Cairo huku matokeo rasmi yakitarajiwa kutangazwa.

Wachambuzi wa siasa za Kimataifa wanaona kuwa kazi kubwa ya Al sisi itakuwa ni kuhubiri msamaha na maridhiano.

Sisi, ambaye alistaafu jeshi ili kugombea nafasi hiyo anakuwa raisi wa tano wa Misri kutoka jeshini kuongoza taifa hilo la akiarabu lenye wakazi wengi zaidi.

Sisi anaingia mamlakani akiwa na wafuasi wengi wanaoamini atarejesha amani na kufufua uchumi baada ya miaka mitatu ya misuguano.