KENYA-Mazingira-Usalama

Mkutano wa mazingira wa kimataifa kufanyikia Nairobi licha ya changamoto za kiusalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon,ni miongoni mwa viongozi watakaohudhuria Mkutano wa Mazingira
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon,ni miongoni mwa viongozi watakaohudhuria Mkutano wa Mazingira REUTERS

Umoja wa Mataifa UN umetangaza kuwa utaandaa mkutano wake wa Mazingira jijini Nairobi nchini Kenya mwezi ujao utakaohudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki Moon licha ya nchi hiyo kukabiliwa na changamoto za kiusalama.

Matangazo ya kibiashara

Ban Ki Moon ataungana na zaidi ya Mawaziri 100 wa Mazingira kutoka Mataifa mbalimbali duniani na zaidi ya watalaam wa mazingira elfu moja kuzungumzia maswala ya mazingira duniani.

Mkutano huo umepangwa kufanyika kati ya tarehe 23 na 27 mwezi ujao katika Makao Makuu ya tume inayoshughulikia mazingira ya UNEP yaliyopo jijini Nairobi.

Huu utakuwa ni mkutano wa kwanza wa mazingira kuwahi kufanyika jijini Nairobi na Naibu Katibu Mkuu wa tume inayoshughuilikia mazingira katika Umoja wa Mataifa Achim Steiner amesema mkutano huo utaendelea licha ya changamoto za kiusalama kutoka kwa kundi la AL Shabab.

Viongozi wengine watakaohudhuria mkutano huo ni pamoja ni Prince Albert wa pili wa Monaco, na rais wa baraza la Umoja wa Mataifa.

Huu ndio mkutano mkubwa wa Umoja wa Mataifa ambao hujadili hatua mbalimbali za kuimarisha uhifadhi na kukabiliana na mazingira duniani.