DRCongo-mauaji

Mazishi ya wahanga wa mauaji ya Mutarule yafanyika wakati hali ikiendelea kuwa tete

Waathirika wa mauaji ya Mutarule mkoani Kivu ya Kusini
Waathirika wa mauaji ya Mutarule mkoani Kivu ya Kusini

Shughuli za mazishi ya watu zaidi ya thalathini waliouawa katika mapigano ya kikabila katika kijiji cha Mutarule karibu na Luberizi kwenye bonde la Ruzizi jimboni kivu ya Kusini yamefanyika jana siku ya Jumapili baada ya kutokea mauaji siku ya Ijumaa yaliotekelezwa na watu waliobebelea silaha na ambapo idadi ya waliopoteza maisha ilifikia watu 36. Vujana wa Mutarule waliokuwa na hasira walizuia barabara ya kitaifa numbari 5 inayounganisha Uvira na Bukavu. Hali hiyo imeshuhudiwa pia tarafani Uvira katika taraja la mto Mulongwe.

Matangazo ya kibiashara

Miili ya watu walipoteza maisha hadi siku ya Ijumaa ilikuwa bado ikielea katika barabara za Mutarule, vijana wenye hasira walipinga kuruhusu miili hiyo kutolewa barabarani wakidai ujio wa viongozi wakuu kabla ya kuruhu miili hiyo kuzikwa.
Barabara hiyo ya kitaifa nambari 5 imefungwa kutwa nzima huku kukiwa na hali ya wasiwasi na shughuli za mazishi zimefanyika baadae mchana

duru kutoka katika eneo hilo zimethibitisha uwepo wa spika wa bunge la Mkoa, Emile Baleke aliyechaguliwa kutoka katika tarafa ya Uvira, waziri wa Mkoa wa Mambo ya ndani pamoja na yule wa usafiri na mawasiliano, lakini pia muakilishi wa kanisa la Pentecote Pasta Jean Miruho Ngombera.

Pasta Miruho amewatolea wito wananchi wa eneo hilo kuendelea kueshi kwa maelewano na kumaliza taofauti zao huku wakitafuta suluhusu ya migogoro kwa njia ya maelewano.

Akiwa Bukavu, mfalme wa watu wa kabila la Barundi amelaumu mauji hayo, na kufahamisha kwamba wahusika watahukumiwa baada ya kugundulika katika uchaguzi. Watu walioendesha mashambulizi walizingira kanisa la Cepac Mutarule kabla ya kuanza kuwashambulia waumini.

Kwa mujibu wa viongozi wa kimkoa wamesema tayari uchunguzi umeanzishwa ili kubaini wahusika wa mauji hayo ya kinyama.

Watu 36 wamepoteza maisha katika vijiji vya Mutarule na Nyamugali pamoja na Katekama katika usiku wa wa Ijumaa kuamkia Jumamosi mwishoni mwa juma lililopita na watu wenye silaha. Duru za awali zilizotolewa na kanisa ziliarifu watu 30 walipoteza maisha na wengine 24 waliojeruhiwa, washambuliaji hao waliteketeza majumba kadhaa likiwemo kanisa walimo kuwepo waumini hao kabla ya kutokomea.

Mutarule inapatikana kwenye umbali wa kilometa 50 kusini mwa Bukavu, kwenye mpaka karibu na Burundi. Duru kutoka katika eneo hilo zimearifu kuwa waliouawa ni watu wa kabila la Bafuliru waliouawa kwa risase na kukakatwa kwa mapanga wakati wakiwa usingizini kanisani baada ya kufanyika kwa ibada ya pamoja mchana kutwa katika kanisa la ki protestanti

 

Shirika la Umoja wa Mataifa nchini DRCongo Monusco limelaani vikali mauaji hayo na kuorodhesha idadi ya watu zaidi ya thalathini waliojeruhiwa katika bonde la Ruzizi, Uvira na Bukavu. Katika taarifa iliotolewa mwishoni mwa juma lililopita mkuu wa Monusco Martin Kobler ameomba kukomeshwa mara moja kwa machafuko hayo.

Vikosi vya Monusco vinasaidia jeshi la FARDC kuhakikisha hali ya usalama na utulivu vinarejea katika eneo hilo. Vikosi vya Monusco vimesaidia pia kuwasairisha majeruhi kuwapelekea Hospitalini.