Mauaji ya watu zaidi ya thelathini mashariki mwa DRC, pamoja na bajeti za nchi za jumuia ya afrika mashariki kusomwa ni Habari muhimu za kiafrika zilizochukua Uzito kwa juma hili.

Sauti 21:34
Askari wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo katika operesheni za kijeshi, mashariki mwa DRC Oktoba 16, 2013,
Askari wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo katika operesheni za kijeshi, mashariki mwa DRC Oktoba 16, 2013, REUTERS/Kenny Katombe

Juma hili kuliripotiwa Makabiliano makali kati ya Wanajeshi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na wanajeshi wa rwanda katika kijiji cha Kanyesheza, kilomita 20eneo la kaskazini mwa jiji la Goma mji mkuu wa mkoawa Kivu kaskazini.Wanajeshi hao walishambuliana kwa zana nzito za kivita, kwa mujibu wa mwanahabari wetu aliye mashariki mwa nchi hiyo.Raisi Salva Kiir wa sudan kusini aahidi kuunda serikali ya muungano wa kitaifa, mawaziri wa fedha wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamesoma bajeti ya 2014/2015 za nchi zao mbele ya wabunge.Na Kimataifa tunaangazia michuano ya fainali za kombe la dunia ambapo timu ya soka ya Brazil ilianza vyema mashindano ya kombe la dunia baada ya kuilaza timu ya taifa ya Croatia mabao matatu kwa moja katika mechi ya ufunguzi iliyofanyika kwenye uwanjwa wa corinthians mjini Sao Paulo.Ungana nami Reuben Lukumbuka, kupata mengi zaidi, Karibu,............