MISRI

Mahakama ya Misri yawataja wanaume 13 kuhusika kuwashambulia wanawake kingono

Wanawake wakiwa katika maandamanokupinga mashambulizi ya ngono dhidi yao jana  Jumamosi Juni 14 2014
Wanawake wakiwa katika maandamanokupinga mashambulizi ya ngono dhidi yao jana Jumamosi Juni 14 2014 REUTERS/Asmaa Waguih

Mahakama nchini Misri imewataja wanaume 13 kuhusika na madai ya mashambulizi ngono dhidi ya wanawake kwenye uwanja wa Tahrir jijini Cairo, ikiwa ni pamoja na wakati wa sherehe za kuapishwa kwa rais mpya Abdel Fattah al-Sisi. 

Matangazo ya kibiashara

Hayo ni mashtaka ya mara ya kwanza kufanywa katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini kuhusiana na mashambulizi ya ngono kwa umma

Ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu imearifu kuwa mashambulizi yalifanyika mnamo Januari 25, 2013, wakati Misri ikiadhimisha miaka miwili ya mapinduzi ya mwaka mwaka 2011, na Juni 3 na Juni 8 mwaka huu wakati raia wakishanglia ushindi na kuapishwa kwa Sisi.

Watuhumiwa 13, ikiwa ni pamoja na madogo, wanashtakiwa kwa utekaji nyara, ubakaji, kushambulia kingono, na kujaribu kufanya mauaji na kutesa wanawake.

Ikiwa watapatikana na hatia, washitakiwa hao wanaweza kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Tangu mapigano yaliyompindua rais wa muda mrefu Hosni Mubarak mwaka 2011, tatizo la unyanyasaji wa kijinsia limekuwa likikithiri zaidi nchini Misri, pamoja na wanawake kushambuliwa na makundi ya wanaume mara kwa mara wakati wa mikutano ya ndani na nje ya Tahrir Square, kitovu cha maandamano.
 

Mamia ya wanawake waliandamana jana Jumamosi mjini Cairo kupinga mashambulizi hayo.