Misri

Mwandishi wa Habari wa Al Jazeera aachiwa huru

Mwandishi wa Habari wa aljazeera Abdullah Elshamy, baada ya kuachwa huru kwake
Mwandishi wa Habari wa aljazeera Abdullah Elshamy, baada ya kuachwa huru kwake REUTERS/Stringer

Hatimaye Mwandishi wa habari wa Al Jazeera Abdullah Elshamy ameachiliwa huru na kuondoka gerezani nchini Misri alikokuwa anazuiliwa kwa muda wa miezi 10 bila ya kufikishwa Mahakamani. 

Matangazo ya kibiashara

Elshamy amekuwa akizuiliwa jijini Cairo na kuanzi mwezi Januari mwaka huu alianza mgomo wa kula kushinikiza kuachiliwa huru na serikali ya Misri ambayo ilikuwa inamtuhumu kushrikiana na kundi la Muslim Brotherhood bila ya kumfungulia mashtaka.

Siku ya Jumatatu kiongozi wa Mashtaka alimuaru kuachiliwa kwake kwa sababu ya kudorora kwa hali yake ya kiafya.

Waendesha mashtaka waliitaka korti kutoa hukumu kali angaa kifungo cha miaka 15 gerezani kwa washukiwa, ambao walikana mashitaka.

Familia ya mwandishi huyu wa habari ililiambia shirika la habari la AFP mwezi Mei kuwa alikuwa amepoteza kilo 40 tangu alipoanza mgomo wa chakula.

Elshamy amesema ataendelea kupigania haki na kuzuiliwa kwake kumebadilisha maisha yake.

Mbali na Elshamy wanahabari wengine wa Al jazeera Peter Greste, Baher Mohamed na Mohamed Fahmy bado wanazuiliwa kwa tuhuma za kushirikiana na kundi la Muslim Brotherhood ambalo serikali inasema ni la kigaidi.

Wanahabari hao walikamatwa wakati polisi walitawanya maandamano yaliyokuwa yakifanywa na waandamanaji wanaomuunga mkono raisi aliyeondolewa madarakani, Mohammed Morsi.