Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mauaji ya Mpeketoni kuzua tafrani nchini Kenya, Kimataifa siasa za mwenyenguvu mpishe Ukraine kuota mizizi.

Sauti 21:26
Wakaazi wa mji wa Mpeketoni Pwani ya Kenya wakishangazwa na mashambulizi yaliyotekelezwa na kundi la Al Shabaab Juni 16 2014.
Wakaazi wa mji wa Mpeketoni Pwani ya Kenya wakishangazwa na mashambulizi yaliyotekelezwa na kundi la Al Shabaab Juni 16 2014. REUTERS/Joseph Okanga

Barani Afrika miongoni mwa mengi yaliyojitokeza ni pamoja na mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika mji wa Mpeketoni pwani ya Kenya ambapo watu wasiopungua sitini walipoteza maisha, wakati huko nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo mamia ya watu waliotekzwa nyara na kundi la waasi wa uganda la ADF ni suala ambalo bado linazua kizungumkuti, pia katika uga wa kimataifa katika juma hili, tunaangazia nchi ya Irak ambako wapiganaji wa kijihadi wameendelea na mapigano wakilenga udhibiti wa miji kadhaa nchini humo, kitu kilichoipelekea kuamua kutuma wanajeshi wake 300, kuisaidia serikali ya nchi hiyo. Ungana nami Reuben Lukumbuka, kupata mengi zaidi.