UGANDA

Waandamanaji waliotumia nguruwe kupinga rushwa nchini Uganda watupwa rumande

Nguruwe hawa walitumiwa katika maandamano kupinga mshahara wa wabunge  nchini Kenya
Nguruwe hawa walitumiwa katika maandamano kupinga mshahara wa wabunge nchini Kenya chimpreports

Wanaume wawili nchini Uganda ambao waliwapenyeza watoto wa nguruwe katika bunge la taifa hilo kupinga rushwa wamepelekwa gerezani kusubiri kesi yao mnamo Julai 4, na wanyama waliotumika kama ushahidi, jamaa zao wamethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Richard Sebuliba, jamaa wa mmoja wa wanaume hao, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa wakiwa mahakamani, hakimu aliwasomea mashtaka matatu ya makosa ya jinai ambayo ni , kufika eneo la bunge kinyume na taratibu,kula njama ya kuwapenyeza nguruwe bungeni na kuingilia shughuli za bunge.
Viongozi wanasema waandamanaji hao waliwapaka nguruwe hao rangi ya chama tawala cha Rais Yoweri Museveni, mmoja wa viongozi wa muda mrefu barani Afrika, na waliandika juu ya wanyama hao kauli mbiu zilizowatusi wabunge kuwa wala rushwa.

Msemaji wa polisi Polly Namaye amethibitisha kukamatwa kwa wawili hao na kuwekwa rumande na kwamba nguruwe wamehifadhiwa chini ya ulinzi wa polisi

Wawili hao Robert Mayanja na Norman Tumuhimbise ni wafuasi wa vuguvugu la maandamano wanaojiita Jobless brotherhood ambao walikuwa wanapinga kile wanachosema ni rushwa na matumizi makubwa yanayofanywa na wabunge nchini humo.

Uganda imekuwa ikikosolewa mara kwa mara na wafadhili wa kigeni kuhusu tuhuma za rushwa ingawa maandamano nchini humo hutokea mara chache.

Mapema mwaka huu wabunge walisababishwa dhoruba baada kuibuka wakidai kuongezewa mishahara ambayo tayari ni mikubwa zaidi mara 60 ya mishahara ya wafanyakazi wa umma na kwamba mkaguzi mkuu waserikali amelalamika kwamba wabunge wameshindwa kuwajibika kutokana na gharama za mamilioni ya dola.