Mauritania-Uchaguzi

Kura za uchaguzi wa raisi zahesabiwa Mauritania wakati huu Abdel Azizi akitarajiwa kushinda

Misururu michache ilionekana katika siku ya kupiga kura mjini Nouakchott
Misururu michache ilionekana katika siku ya kupiga kura mjini Nouakchott Marie-Pierre Olphand

Bado zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Mauritania,baada ya kukamilika kwa upigaji kura hapo jana uchaguzi ambao rais wa sasa, Mohamed Ould Abdel Aziz anatarajiwa kushinda kirahisi.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu umefanyika wakati ambapo upinzani ulisusia kushiriki, kwa madai ya kuwa mchakato mzima wa maandalizi ya uchaguzi huu haukuwa huru na haki na kwamba ulilenga kumpendelea rais Abdel Aziz.

Misururu mifupi ya watu ilionekana katika vituo vingi vya kupigia kura kwenye mji mkuu, Nukchott, huku viongozi wa chama tawala na waangalizi toka Umoja wa Afrika wakigusia kuwa zoezi lilienda vizuri licha ya kasoro zilizoripotiwa na upinzani.

Kwenye kampeni zake rais Abdel Aziz aliwataka wananchi wamchague tena ili amalizie shughuli ya kuyakabili makundi ya kigaidi nchini humo.