JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Watu zaidi ya 50 wauliwa katika mapigano mapya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kambi ya wakimbizi Bambari
Kambi ya wakimbizi Bambari © EU/ECHO/Patrick Lambrechts

Jeshi la Umoja wa Afrika la kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati linasema zaidi ya watu 50 wameuliwa katika mapigano mapya kati ya Wakiristo na Waislamu nchini humo kwa kipindi cha siku tatu zilizopita.

Matangazo ya kibiashara

Mauaji haya yalizuka baada ya ripoti za kuuliwa kwa Waislamu 17 katika kambi ya wakimbizi ya Bambari siku ya Jumatatu juma hili na kundi la waasi la Wakiristo la Anti-Balaka.

“Watu zaidi ya 50 wameuliwa tangu siku ya Jumatatu katika jimbo la Bambari na vijiji vingine,” Mwanajeshi wa Umoja wa Afrika ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa la AFP.

“Idadi kubwa ya waliouliwa walipigwa risasi au kudungwa visa hadi kufa. ,”
Jeshi la kulinda amani nchini humo MISCA linasema tangu mapema juma hili, kumekuwa na mauaji ya kuvizia na kulipiza kisasi kati ya Wakiristo na Waislamu nchini humo.

“Mbali na mauaji hayo yanayowalenga raia wa kawaida, makaazi yao yanateketezwa moto na wengi wao ambao ni Wakiristo wanakimbilia Kanisani na katika makaazi ya Askofu.,” Mwanjeshi mwingine ambaye hakutaka kutajwa amesema.

Wanajeshi wa Ufaransa wakifungua barabara jijini Bangui
Wanajeshi wa Ufaransa wakifungua barabara jijini Bangui AFP PHOTO/MARCO LONGARI

Mapigano haya ya hivi punde yanakuja, siku moja tu baada Mashirika ya kutetea haki za Binadamu nchini humo FIDH kusema visa vya ukiuwkaji wa haki za binadamu vinatekelezwa nchini humo.

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika wakimpa ulinzi mwanamke nje ya jiji la Bangui
Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika wakimpa ulinzi mwanamke nje ya jiji la Bangui REUTERS/Siegfried Modola

Ripoti ya mashirika hayo iliyopewa jina “ Ni sharti waondoke wote au wafe”, inaeleeza kuwa kinachotokea nchini humo ni mapambano ya kutaka madaraka ambayo yamechukua mrengo wa kidini kati ya Wakiristo na Waislamu nchini humo.

Tangu mwezi Desemba mwaka 2013 jijini Bangui, wapiganaji wa Anti- Balaka wamekuwa wakitekeleza mauaji dhidi ya Waislamu nchini humo kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Kundi la Wailsmau la Seleka pia bado linaendelea kutekeleza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Ripoti hiyo inamtaja  rais wa zamani Michel Djotodia, aliyekuwa Mkuu wa kitengo chake cha Inteljensia Noureddine Adam na kiongozi wa kundi la wapigaji wa Janjaweed nchini Sudan Jenerali Moussa Assimeh kuhusika moja kwa moja na mauaji nchini humo.