Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Hukumu dhidi ya waandishi wa kituo cha Aljazeera, pia hali ya ulaji wa Nyama za binadamu huko DRC, kama habari kuu barani Afrika kwa juma hili

Sauti 21:16
MISRI
MISRI RFI

Ni mengi yaliyojitokeza kwa juma hili barani Afrika, ikiwa ni pamoja na hukumu iliyotolewa na mahakama moja nchini Misri dhidi ya Wanandishi wa Habari wa kituo cha Aljazeera, wakati nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufanyika vitendo vya kula nyama ya binadamu kulilaaniwa vikali na Jumuia ya kitaifa, Kuachiwa huru kwa mwanamke aliyekuwa ameasi uisilamu na kuolewa na mkristo huko Sudan; hukumu aliyopewa na masaibu aliyoyapitia, lakini pia Hali ya mivutano ya kisiasa kati ya Syria na Marekani, na hatimaye hali ya mambo huko Ukraine.Karibu Kuungana nami Reuben Lukumbuka.