SOMALIA-AL SHABAB-Ugaidi-Usalama

Kundi la Al Shabab laonya kuendeleza mashambulizi Somalia

Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab nchini Somalia.
Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab nchini Somalia. REUTERS/Feisal Omar

Kundi la wanamgambo wa Al-Shabab nchini Somalia limekiri kuhusika na mfululizo wa mashambilizi ya mabomu kwenye mji mkuu Mogadishu na kuonya kuwa litaendelea na mashambulizi haya hata wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa kundi hilo, Abdulaziz Abu Musab amethibitisha wapiganaji wake kutekeleza mashambulizi matano ya mabomu Jumatatu ya wiki huu kwenue mji wa Mogadishu na kuapa kuzidisha mashambulizi yao wakati huu wa mfungo.

Wapiganaji wa kundi la Al Shabab katika kambi yao ya mazoezi nchini Somalia.
Wapiganaji wa kundi la Al Shabab katika kambi yao ya mazoezi nchini Somalia. Reuters / Feisal Omar

Licha ya usalama kuimarishwa kati ya vikosi vya Serikali na vile vya kulinda amani ncini humo AMISOM, wachambuzi wa masala ya usalama wanaona hali bado ni tete nchini Somalia na usalama inabidi kudhibitiwa kama anavyoeleza hapa Mwenda Mbijiwe akiwa jijini Nairobi nchini Kenya.