SUDANI KUSINI-Mapigano-Usalama

Sudani Kusini : mapigano yazuka katika mji wa Nasir

Wanajeshi wa Sudani Kusini watiifu kwa Salva Kiir, kwenye uwanja wa ndege wa Bor, kilomita 200 na mji wa Juba.
Wanajeshi wa Sudani Kusini watiifu kwa Salva Kiir, kwenye uwanja wa ndege wa Bor, kilomita 200 na mji wa Juba. REUTERS/Andreea Campeanu

Mapigano yameendelea jumatatu wiki hii katika mji mdogo wa Nasir, kaskazini mashariki mwa Sudani Kusini, siku moja kabla ya kuanza kwa mashambulizi ya nayoendeshwa na waasi katika ngome yao ya zamani, ofisi ya Umoja wa Mataifa katika mji huo imelithibitishia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Matangazo ya kibiashara

“Mapigano yanaripotiwa ndani ya mji” msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa, Joe Contreras. “Mapigano hayo yako upande wa pili karibu na kambi ya wanajeshi wa Sudani Kusini, magharibi mwa mji”, ameendelea kusemamsemaji wa UNMISS.

“Waasi wanashikilia kwa sasa eno la katikati ya mji la Nasir”, katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Nil, laikini jeshi bado lipo, ameongeza, huku akibaini kwamba ni vigumu kusema kwamba mji umetoka mikononi mwa jeshi na kushikiliwa kwa sasa na waaasi.

Mpiganaji wa kundi la waasi linaloongozwa na Riek Machar, katika mji wa Bentiu, Sudani Kusini.
Mpiganaji wa kundi la waasi linaloongozwa na Riek Machar, katika mji wa Bentiu, Sudani Kusini. REUTERS/Emre Rende

Waasi walithibitishwa jumapili jana kwamba wameushikilia mji wa Nasir, ambao unapatikana kwnye umabli wa kilomita 500 kusini mwa Juba, karibu na mpaka na Ethiopia.

Eneo la Nasir lilikua ngome ya waasi wanaoongozwa na aliekuwa makamu wa rais Riek Machar, kabla ya jeshi linalomuunga mkono rais Salva Kiir kulirejesha kwenye himaya yake, May 4 mwaka 2014.

Iwapo Nasir itakua mikononi mwa waasi, itakua ni eneo la kwanza muhimu kushikiliwa mara kadhaa na pande zote mbili (jeshi na waasi) tangu rais Salva Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar kukutana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, ambapo waliafikiana kusitisha mapigano, hatua ambayo haijatekelezwa hadi sasa.