CAR-CONGO-SELEKA-ANTIBALAKA-Maridhiano

CAR : Congo : wakuu wa kijeshi wa Seleka wawasili Brazzaville

Mkutano kuhusu namna ya kuboresha maridhiano na mazungumzo kati ya makundi hasimu na wanasiasa wazinduliwa katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville.
Mkutano kuhusu namna ya kuboresha maridhiano na mazungumzo kati ya makundi hasimu na wanasiasa wazinduliwa katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville. AFP PHOTO/GUY-GERVAIS KITINA

Viongozi tisa wa kijeshi wa kundi la zamani la wasaa la Seleka wamewasili jana jumanne jioni mjini Brazzaville ili kujaribu kupatia ufumbumbuzi mazungumzo ya amani kwa taifa la Jamhuri ya Afrika ya Kati yanayoendelea nchini Congo, baada ya kukwama kwa siku ya jana, chanzo rasmi mchini Congo kimefahamisha

Matangazo ya kibiashara

“Wakuu tisa wa kijeshi wa Seleka wamewasili jioni ya jumanne wiki hii mjini Brazzaville”, mshauri wa rais Denis Sassou Nguesso anaehusika na msuala ya ufundi ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

“Uamzi wa kwenda kuwatafuta watu hao mjini Bangui ni hatua ya pili”, afisa mmoja kwenye wizara ya mambo ya nje ya Congo ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Mkutano kuhusu maridhiano ya kitaifa na mazungumzo ya kisiasa nchini Jamhuri ya Afrika Kati ulianza jumatatu na kuendelea hadi jana jumanne mjini Brazzaville, ambapo kiongozi wa ujumbe wa Seleka, Mohamed-Moussa Dhaffane, ametoa sharti la kukubali kuligawa taifa hilo kabla ya mazungumzo yoyote kuanza.

Hapo jana jumanne, wajumbe wa Seleka walikataa kushiriki mazungumzo hayo na kuamua kusalia hotelini walikofikia. Kutokana na kutoshiri kwa wajumbe wa Seleka, shughuli ziliyokua zimepangwa kuhusu kusitisha kwa machafuko na suala la kupokonya silaha makundi yanaozimiliki kinyume cha sheria zilisimamishwa baada tu ya ufunguzi wa kikao. Shughuli hizo ziliendelea jioni, bila hata hivo ushiriki wa Seleka.

Viongozi wa nchi ya Congo, wanaoandaa mkutano huo kwa niaba ya Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika ya Kati (CEEAC) walisema jana kwamba waliamua kuahirisha mkutano huo hadi pande zote zitakubaliana kusitisha machafuko, na kuweka saini kwenye mkataba wa usitishwaji machafuko, na baadae mkataba kuhusu kupokonya silaha makundi yenye silaha.

Tangu kupinduliwa kwa rais François Bozizé na waasi wa Seleka, ambao wengi wao ni kutoka jamii ya waislamu, Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo ni tajiri kwa madini mbalimbali, iliingia katika vita vya kikabila, ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na mamia wengine kuyahama makaazi yao.

Waasi wa zamani wa Seleka na wanamgambo kutoka jamii ya wakristo antibalaka wamekua wakihasimiana hadi kusababisha maafa nchini Jamhuru ya Afrika ya Kati.