UINGREZA-MSF-VIRUSI VYA EBOLA-Afya

Uingereza : virusi vya Ebola tishio kwa ulimwengu

wauguzi wakijiandaa kutoa huduma ya kimatibabu kwa wagonjwa wa maradhi ya Ebola, nchini Guinea.
wauguzi wakijiandaa kutoa huduma ya kimatibabu kwa wagonjwa wa maradhi ya Ebola, nchini Guinea. AFP PHOTO / MEDECINS SANS FRONTIERES

Hofu ya kuenea kwa virus vya Ebola katika mataifa mengine duniani imetanda duniani kote, baada ya virusi hivyo kuendelea kushika kasi katika mataifa ya magharibi mwa Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Uingereza wamechukua tahadhari dhidi ya virusi hivyo vya Ebola, huku Hong Kong ikiwa tayari imekwisha hatua za kujilinda dhidi ya virusi hivyo.

Shirika la Madaktari wasio na Mipaka (MSF) limetoa onyo dhidi ya virusi vya Ebola, ambavyo vimesababisha vifo vya watu 670 katika baadhi ya mataifa ya Afrika ya mashariki, shirika hilo likibaini kwamba mataifa hayo hayakujidhatiti vilivyo kwa kukabiliana na virusi hivyo.MSF imesema inatiwa hofu na mataifa mengine kukabiliwa na virus vya Ebola.

Mataifa ambayo yameshaguswa na virusi vya Ebola, ni Guinea, Liberia, Sierra Leone na Nigeria ambapo abiria mmoja amewasili katika mji wa Lagos kwa ndege akitokea katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia, kufariki baada ya kuambukizwa virusi hjivyo. Tayari mashirika mawili ya ndege kutoka bara la Afrika Arik na ASKY yamesitisha safari zao katika nchi za Liberia na Sierra Leone kufuatia hali hiyo.

Mataifa ya ulaya na Afrika yamekua na hofu na kusambaa kwa virusi vya Ebola.
Mataifa ya ulaya na Afrika yamekua na hofu na kusambaa kwa virusi vya Ebola. AFP PHOTO / SEYLLOU

Shirikisho la kimataifa la usafiri wa anga (OACI) limekutana kwa mazungumzo na shirika la Afya Dunia kujadili kuhusu virus hivyo vy Ebola, bila hata hivo kubaini ni mikakati gani ambayo wamo mbiyoni kufanya ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Ebola katika mataifa ambayo hayajakumbwa na maradhi hayo.

Nchini Uingereza, vikao mbalimbali kupitia wizara mbalimbali vimeandaliwa kuhusu jinsi gani watakabiliana na virusi vya Ebola, huko viongozi wakisema kutiwa hofu na virusi hivyo.

Wataalamu wamebaini kwamba kutapika, kuharisha na kutokwa na damu kwa wingi kinywani, puani na sehemu zingine za siri ni miongoni mwa ishara za virusi vya Ebola. Wataalamu hao wamebaini pia kwamba maradhi ya Ebola hayana kinga na yanaua kwa asilimia kati ya 25 na 90.