SUDANI KUSINI-Baa la njaa-Usalama

Sudani Kusini: raia wakabiliwa na baa lanjaa, mazungumzo ya amani yaanza

Mazungumzo ya kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudani Kusini yataanza tena Ogasti 4, wasuluhishi wamethibitisha ijumaa wiki hii, wakati baa la njaa limekua ni tishio kwa taifa hilo changa la Sudani Kusini linalokabiliwa na machafuko.

Raia wa Sudani Kusini wakabiliwa na baa la njaa, huku mapigano yakiendelea.
Raia wa Sudani Kusini wakabiliwa na baa la njaa, huku mapigano yakiendelea. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo ambayo yangelianza wiki hii, hatimaye yataanza jumatatu wiki ijayo, wamethinbitisha viongozi wa jumuiya ya maendeleo ya Afrika Mashariki, IGAD, ambao wanasimamia mazungumzo hayo.

Mashirika ya kutoa misaada ya kiutu nchini Sudani Kusini na yale ya kimataifa yamebaini kwamba baa la njaa litakua ni tishio siku za usoni iwapo mapigano hayatasitishwa.

Raia wa Sudani Kusini waliyopewa hifadhi katika kambi iliyojengwa katika eneo la Umoja wa Mataifa.
Raia wa Sudani Kusini waliyopewa hifadhi katika kambi iliyojengwa katika eneo la Umoja wa Mataifa. REUTERS/UNMISS/Handout via Reuters

IGAD, ambayo inasimamia mazungumzo hayo imesema kwamba mazungumzo kati ya amani nchini Sudani Kusini yalichelewa kuanza kutokana na likizo ndefu.

Mazungumzo kati ya rais Salva Kiir na aliekua makamu wake Riek Machar yaligonga mwamba mwezi Juni, huku kila mmoja akitupia lawama mwengine kuwa chanzo cha mazungumzo hayo kukwama.

Machafuko hayoyaliyochochea kisiasa na kikabila yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na zaidi ya watu milioni 1.5 wameyahama makaazi yao.

Mazungumzo ya awali yaliyofanyika katika hoteli za kifahari za mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa yaligharimu Dola miilioni 17 (sawa na Uro milioni 12), bila hata hivo kuzaa matunda yoyote, kwani mikataba mitatu ya kusitisha mapigano iligonga mwamba.