KENYA-UPINZANI-Siasa-Haki za binadamu

Kenya: serikali yatetea uamzi wake

Makamu wa rais wa Kenya, William Ruto ameendelea kusisitiza msimamo wa serikali ya nchi hiyo kuhusu hatua waliyoitangaza juma moja lililopita ya kuwapokonya ardhi watu binafsi na makampuni yanayodaiwa kunyakua ardhi kwa nguvu kwenye mji wa Lamu pwania ya Kenya.

Makamu wa rais William Ruto asema serikali yake haitorudi nyuma wala kutishika kwa uamzi iliyochukua
Makamu wa rais William Ruto asema serikali yake haitorudi nyuma wala kutishika kwa uamzi iliyochukua REUTERS/Lex van Lieshout/Pool
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya makamu wa rais, Ruto ameitoa akijibu hoja zinazotolewa na upinzani ambao unataka serikali kuachana na mpango huo na kwamba utachukua hatua za kisheria kupinga uamuzi wa Serikali, msimamo ambao naibu wa rais Ruto anasema serikali yake haitorudi nyuma wala kutishika.

Makamu wa rais William Ruto anasema kuwa ni kitendo cha kustaajabisha na kilichopitwa na wakati kuona viongozi wa upinzani wanatumia muda mwingi kutoa vitisho dhidi ya Serikali na kuongeza kuwa vitisho hivi havisaidii.

Makamu wa rais Ruto, aanatoa kauli hii wakati ambapo hii leo tume ya ardhi nchini humo inatarajiwa kuanza kutekeleza agizo la rais Uhuru Kenyatta kuchukua ardhi inayokadiriwa kufikia hekari laki 5ambayo ilikuwa inamilikiwa kinyume cha sheria.