Marekani: Barack Obama ataka ushirikiano wa kina na bara la Afika
Serikali ya Marekani imewataka viongozi wa bara la Afrika kuheshimu tofauti za kisiasa zilizoko nchini mwao na kuwa na uvumilivu wa kisiasa ambao ndio nguzi kuu ya kuwa na demokrasia ya kweli katika kufikia mafanikio ya muda mrefu.
Imechapishwa:
Wito huu umetolewa wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya viongozi hao na rais Barack Obama, ambaye alitumia siku ya kwanza ya mkutano huu, kusisitiza masuala ya usalama, biashara na demokrasia kama msingi mkuu utakaoshuhudia nchi za Afrika zikipata maendeleo ya haraka.
Kuhusu biashara, rais Obama amesema kuwa haoni shida nchi ya China kuwa mwekezaji mkubwa barani Afrika lakini akaonya kuhusu uwekezaji unaofanywa na taifa hilo na kuwataka viongozi hao kuwa makini na rasilimali ambazo China imekuwa ikizilenga kwenye bara hilo.
Viongozi wa mataifa hamsini na Umoja wa Afrika wamealikwa. Hata hivo Jamhuri ya Afrika ya Kati, Zimbabwe, Soudani na Erythrea hazikupata mualiko. Rais wa Marekani anafanya mkutano huu ili kuanzisha uhusiano wa Marekani na bara nzima la Afrika.
Naibu mshauri wa masuala ya usalama na mawasiliano wa rais Barack Obama, Benjamin Rhodes, amesisitiza kile ambacho kilisemwa na rais Obama wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.