BENKI KUU YA DUNI-EBOLA-AFRIKA-Afya

Benki ya Dunia yajiandaa kupambana na ugonjwa wa Ebola

Wakati dunia ikiendelea na harakati za kukabiliana na maambukizi zaidi ya virusi vya ugonjwa wa Ebola, benki ya dunia imetangaza kutoa kiasi cha dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Benki ya Dunia yaetangaza kutoa kiasi cha dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola.
Benki ya Dunia yaetangaza kutoa kiasi cha dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola. AFP PHOTO / MEDECINS SANS FRONTIERES
Matangazo ya kibiashara

Jana jumanne, benki ya dunia imetangaza kutoa kiasi cha dola milioni 200 kwa nchi za Liberia, Guinea na Sierra Leone kusaidia nchi hizi za Afrika Magharibi ambazo zimekumbwa na ugonjwa hatari wa ebola ambao mpaka sasa umeua watu zaidi ya 900 toka ulipobainika mwezi March mwaka huu.

Rais wa Benki ya dunia, Jim Yong Kim ambaye kitaaluma pia ni mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko amesema amekuwa akifuatilia harakati za kukabiliana na ugonjwa huu hatari ambao umeonekana kuwa tishio kwenye nchi hizo tatu na dunia kwa ujumla.

Fedha hizi zitasaidia kununua dawa, kulipa wafanyakazi pamoja na kushughulikia maeneo mengine ambayo yanahitaji fedha kwa ajili ya kukabiliana na mlipuko wa magonjwa ya aina kama hii.

Katika hatua nyingine dawa aina ya Zmapp ambayo iko kwenye majaribio na wamepewa raia wawili wa Marekani, imepelekea raia hao kupata ahueni toka walipoanza kutumia dawa hiyo ambayo kwa mara ya kwanza inafanyiwa majaribio kwa binadamu na tayari imeonesha ishara ya kuwa na nguvu ya kukabiliana na virusi hivyo vya Ebola.