UFARANSA-MALI-ANSAR DINE- Vitisho-Usalama

Iyad Ag Ghali, aionya Ufaransa

Baada ya miezi kadhaa ya utulivu, hatimaye Iyad Ag Ghali, kiongozi wa kundi la wanamgambo wa kislamu la Ansar Dine ameonekana katika mkanda wa video akifanya vitisho vya kuishambulia Ufaransa.

Iyad ag Ghali, kiongozi wa kundi la Ansar Dine, wakati akipokelewa kwa mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Ogasti 7 mwaka 2012.
Iyad ag Ghali, kiongozi wa kundi la Ansar Dine, wakati akipokelewa kwa mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Ogasti 7 mwaka 2012. AFP PHOTO / ROMARIC OLLO HIEN
Matangazo ya kibiashara

Video hiyo ilirushwa kwenye mtandao wa wanamgambo hao wa kislamu Julai 29. Jeshi la Ufaransa lilianzisha operesheni Serval, baada ya kiongozi huyo wa Ansar Dine kukiri kwamba wapiganaji wake ndio waliohusika katika shambulio liliyotekelezwa katika kijiji cha Konna, kaskazini mwa Mali.

Baadhi ya watu walidai kwamba Iyad Ag Ghali, aliiuawa katika operesheni iliyoendeshwa na jeshi la Ufaransa Serval, baada ya kundi la Ansar Dine kutekeleza shambulio katika kijiji Cha Konna.

Wanamgambo wa kundi la Ansar Dine na kiongozi wao, Iyad Ag Ghali, akiendesha ibada ya swala.
Wanamgambo wa kundi la Ansar Dine na kiongozi wao, Iyad Ag Ghali, akiendesha ibada ya swala. Reuters / Ansar Dine

Katika video hiyo, Iyad Ag Ghali, ameonekana akiwa na ndevu ndefu, huku akishikilia silaha mkononi. Iyad Ag Ghali amezungumza kwa muda wa dakika 13 katika mkanda huo wa video unaodumu dakika 24, ambapo aliionya Ufansa akiitohumu kwamba imeanzisha utawala wa kikoloni katika maeneo ya kaskazini mwa Mali.

Iyad Ag Ghali ametangza vita dhidi ya Ufaransa na washirika wake, huku akibaini kwamba wameanzisha harakati za kupambana vilivyo na Ufaransa.

“Tuko tayari kupambana na Ufaransa pamoja na washirika wake”, amesema Iyad Ag Ghali, katika mkanda huo wa video. Ansar Dine ni kundi lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda, na limekua likitekeleza mashambulizi tofauti katika aridhi ya Mali.

Katika mkanda huo wa video, Ufaransa imenyooshewa kidole kwamba inaingilia masuala ya ndani ya taifa la Mali na kudai kwamba imekua Ufaransa imekua ikipora mali za nchi ya Mali, hususan dhahabu, uranium na shaba.

Iyad Ag Ghali, amekiri katika mkanda huo wa video kuhusika katika mshambulizi ya makombora na mashambulizi mengine ya kujitoa muhanga dhidi ya wanajeshi wa Ufaransa waliyoendesha operesheni “Serval”, bila hata hivo kutoa taarifa zaidi.

“Lengo letu sisi ni kuweka sheria ya kislamu katika eneo tunaloshikilia”, amesema Iyad Ag Ghali, huku akipongeza ndugu zake wa makundi ya wanamgambo wa kislamu nchini Nigeria, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Misri, Pakistan na Afghanistan.