MISRI-EGYPTE-Siasa-Uchumi-Diplomasia

Moscow-Cairo: Ushirikiano waendelea kupiga hatua maridhwa

Rais wa Misri Abdel Fattah Al-Sissi yuko katika ziara rasmi aliyoibuni jana nchini urusi, hii ikiwa ndio ziara yake ya kwanza nchini humo tangu kushika hatamu za uongozi wa Misri.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin (kulia) na mwenziye wa Misri, Abdel Fattah Al-Sissi (kushoto) katika mji wa Sotchi, nchini Urusi, Agosti 12 mwaka 2014.
Rais wa Urusi, Vladimir Putin (kulia) na mwenziye wa Misri, Abdel Fattah Al-Sissi (kushoto) katika mji wa Sotchi, nchini Urusi, Agosti 12 mwaka 2014. AFP PHOTO / RIA NOVOSTI / KREMLIN POOL / ALEXEI DRUZHININ
Matangazo ya kibiashara

Rais Sissi alionyeshwa vifaa kadhaa vya kijeshi vilivyokuwa vimewekwa katika uwanja wa ndege mjini Sochi kwa ajili ya kuvikaguwa mara alipowasili mjini Moscow nchini Urusi, Vifaa hivyo vya kijeshi ni pamoja na magari mapya ya deraya na mifumo ya makombora.

Katika mazungumzo yake na wanahabari punde baada ya kukutana na raisi Vladmiri Putin wa Urusi, Sissi amesema amepigwa na butwaa na kuridhika na ushirikiano wa Urusi.

Urusi kupitia ushirikiano  uliopanuliwa  wa kijeshi  na  kiuchumi , imepata  nafasi  kubwa  ya ushawishi  nchini  Misri, ambayo  ni  mshirika  muhimu  wa Marekani  katika  mashariki  ya  kati.

Vladimir Putin na Abdel Fattah Al-Sissi wakiwa ndani ya gari ya kijeshi yenye silaha ya kurusha makombora iitwayo «Moskva» mjini Sotchi, Agosti 12 mwaka 2014.
Vladimir Putin na Abdel Fattah Al-Sissi wakiwa ndani ya gari ya kijeshi yenye silaha ya kurusha makombora iitwayo «Moskva» mjini Sotchi, Agosti 12 mwaka 2014. REUTERS/Alexei Druzhinin/RIA Novosti/Kremlin

Katika kipindi cha miezi sita pekee mwaka 2014 watali nusu milioni kutoka nchini Urusi wameingia nchini Misri. Lakini rais wa Misri, Abdel Fattah Al-Sissi anataka Urusi iwekeze katika sekta ya viwanda na mafuta.

Misri inataka pia makampuni ya gesi ya Urusi yaanzishe zoezi la kuchimba mafuta na gesi, ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa taifa hilo, katika bahari ya Mediterania. Viongozi hao wawili wamezungumzia pia ushirikiano katika masuala ya nuklia.