PALESTINA-ISRAELI-MISRI-HAMAS-Usalama

Palestina : Gaza : makubaliano ya kusitisha vita yaongezwa muda wa saa 24

REUTERS/Ibraheem Abu Mustafa

Palestina na Isreali zimekubali kuengeza muda wa saa 24 wa kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza ili kutoa nafasi ya kuendelea na mazungumzo ya kumaliza machafuko kati ya Hamas na Israel.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yanayofanyika katika mji mkuu wa Misri, Cairoyanashirikisha ujumbe wa Israel na ule wa Palestina akiwemo muakilishi wa kundi la Hamas. Palestina imefahamisha kwamba imekubali pendekezo la Misri na inasubiri msimamo wa Baraza la usalama la Israel.

Misri imependekeza pande mbili husika kukubaliana kusitisha mapigano kwa muda wa saa 24. lengo kuu ikiwa ni kujizuia, upande wa Hamas, kurusha makombora katika aridhi ya Israeli, huku Isreali ikitakiwa kuondoa vizuizi ili kurahisisha kupitisha chakula na dawa pamoja na vifaa vingine vya hospitali na kuwapatishia umeme raia wa Gaza.

Baada ya hali ya utulivu kwa muda wa mwezi mmoja, suala la usalama litajadiliwa, hususan kupokonya silaha kundi la Hamas kwa njia moja ama nyingine, ujenzi wa bandari au uwanja wa ndege katika ukanda wa gaza, kubadilishana wafungwa wa kipalestina dhidi ya miili ya wanajeshi wa Israel waliouawa pamoja na ujenzi wa wa ukanda wa Gaza.

Misri imependekeza pia kuwa Ukanda wa Gaza utakua chini ya uongozi wa rais Mamlaka ya Palestina Mahoud Abbas, ambaye utawala wake ulisitishwa mwaka 2007 na kundi la Hamas. Uongozi wa Mamlaka ya Palestina ndi utasimamia masuala ya usalama na kuandaa miradi na gharama zinazo husiana na ujenzi wa ukanda wa Gaza.