LIBERIA-EBOLA-Afya-Usalama

Liberia : serikali yatangaza amri ya kutotembea usiku

Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf ametangaza amri ya kutotembea nyakati za usiku pamoja na kuzuia watu kutoka wala kuingia kwenye vitongoji vitatu kimoja kikiwa mjini Monrovia kwenye eneo la West Point, ikiwa ni hatua inayolenga kukabiliana na maambukizi ya virusi hatari vya Ebola.

Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf.
Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf. DR
Matangazo ya kibiashara

Akiwahutubia wananchi kupitia njia ya Redio, rais Sirleaf amesema kuwa amri hiyo itaanza kufanya kazi leo Jumatano nchi nzima kuanzia majira ya satatu za usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi huku vitongoji vitatu vilivyotajwa kuwa chini ya uangalizi wa wananchi wake wakizuiliwa kutoka wala kuingia.

Jitihada za kupambana dhidi ya Virusi vya Ebola zinaendelea nchini Liberia.
Jitihada za kupambana dhidi ya Virusi vya Ebola zinaendelea nchini Liberia. REUTERS

Kiongozi huyo ameagiza kufungwa kwa maeneo yote ya Starehe ifikapo saa kumi na mbili kamili jioni kuanzia leo na kuendelea.

Katika hatua nyingine, nchi hiyo imepata ahueni, baada ya hapo jana waziri wa habari nchini humo, Lewis Brown kutangaza kurejea kwa wagonjwa wote kumi na saba ambao walitoroka kwenye kituo kimoja mjini Monrovia mwishoni mwa juma baada ya kuvamiwa na kundi la vijana.

Rais Ellen Johnson Sirleaf amesema amri hiyo imeanza kutekelezwa jumatano wiki hii kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi saa za Liberia sawa na saa za kimataifa.

Rais Sirleaf ameamuru pia kufungwa kwa vituo vya burudani na majumba ya starehe kuanzia saa kumi nambili jioni saa za Liberia sawa na saa za kimataifa.

Rais huyo mwanamke wa kwanza nchini Liberia, ameelezea masikitiko yake kushindwa kudhibiti Homa ya Ebola licha ya jitihada zinazofanywa, kutokana na namna raia wa nchi hiyo hawafuati masharti ya kujitenga na ndugu zao wanaoambukizwa virusi vya Ebola, hasa wanapofanya mazishi ya ndugu zao wanaofariki kutokana na Homa ya Ebola.

Hata hivo, mratibu wa masuala ya Homa ya Ebola kwenye Umoja wa Mataifa, daktari david Nabarro, amearifu jumanne wiki hii kwamba atajielekeza wiki hii katika mataifa ya Liberia, Sierra Leone, Nigeria, na Guinea ambayo yanaendelea kukumbwa na Homa ya Ebola kwa lengo la kushinikiza kikosi cha wanajeshi 7,500 wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia kupambana dhdi ya ugonjwa huo hatari.