NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Nigeria: wakimbizi 11,500 wanakabiliwa na ukosefu wa chakula

Watu wanaokadiriwa kufikia elfu 11,500 wamekimbia makazi yao katika mji wa Gwoza katika jimbo la Borno kaskazini mwa Nigeria, mji ambao kwa sehemu kubwa unamilikiwa na wapiganaji wa kundi la Boko Haram, ambapo kwa sasa wanaishi kwenye kambi maalumu, limesema shirika la misaada ya dharura la kitaifa (NEMA).

Uharibifu uliyotekelezwa na kundi la Boko haram katika moja ya soko la Maiduguri, nchini Nigeria.
Uharibifu uliyotekelezwa na kundi la Boko haram katika moja ya soko la Maiduguri, nchini Nigeria. AFP PHOTO/STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa yake, shirika hilo limesema kuwa wanawake na wanaume zaidi ya elfu 11 wamekimbia nyumba zao kuhofia kushambiliwa na wapiganaji wa Boko Haram ambao wamekuwa wakiendesha operesheni za nyumba kwa nyumba kwenye mji huo.

Kundi la wapiganaji wa Boko Haram waliuteka mji wa Gwoza mwanzoni mwa mwezi huu, mji ambao uko mpakani na nchi ya Cameroon wakati huu ambapo jeshi likiendelea na jitihada za kuurejesha kwenye himaya yake.

Raia hao wamejificha kwenye mlima uliyo karibu na mji wa Gwoza, kwa wiki moja saa hawana chakula wala maji, huku wengine wakitembea kwa mguu kwa muda wa siku 4 wakielekea ktika mji wa Maiduguri, makao makuu ya mji wa Borno.

shirika la misaada ya dharura la kitaifa (NEMA) limethibitisha kwamba limeshindwa kuhudumia wakimbizi hao kutokana na hali ya usalama inayojiri katika eneo hilo.