Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Kamati kuu ya chama tawala CCM nchini Tanzania kukutana, Ubakaji kuzidi mashariki mwa DRC, Ziara ya afisa wa UN kuhusu Ebola huko Afrika magharibi.

Imechapishwa:

Habari zilizopewa uzito kwa juma hili kwanza ni mkutano wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi CCM nchini tanzania kujadili juu ya mwenendo wa mchakato wa ndani na nje ya bunge maalum la katiba, na huko nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wataalamu wa afya kutoka shirika la Heal Afrika walitangaza ripoti yao iliyobainisha kuwa wanawake takribani elfu tatu walibakwa kwatika kipindi cha miezi mitatu kuanza mwezi marchi hadi juni mwaka 2014, walibakwa katka mikoa ya Maniema na Kivu Kaskazini.Na katika Afrika magharibi, ziara ya afisa wa umoja wa mataifa anayehusika na ebola kuanza juma hili, huku katika uga wa kimataifa, mataifa ya magharibi kuelezea wasi wasi wao kuhusu kuvuka mpaka kwa malori ya misaada kutoka urusi kuingia Ukraine.Ungana nami Reuben Lukumbuka kupata mengi zaidi. 

Sayari ya dunia
Sayari ya dunia
Vipindi vingine