NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Nigeria: wanajeshi 500 waliokimbilia Cameroon warejeshwa

Des militaires nigérians se préparent à une patrouille nocturne dans la forêt de Sambisa, en partie contrôlée par Boko Haram (avril 2014).
Des militaires nigérians se préparent à une patrouille nocturne dans la forêt de Sambisa, en partie contrôlée par Boko Haram (avril 2014). Ben Shemang / RFI

Wanajeshi mia tano wa Nigeria waliovuka mpaka na kukimbilia katika nchi jirani ya Cameroon jumapili iliyopita, wamerejea nchini Nigeria jumatatu wiki chini ya ulinzi mkali.

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao walivuka mpaka wakati walipokua wakipambana na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia vya Nigeria katika mji mkuu wa Cameroon, Yaounde, wanajeshi hao walijiondoa kwenye mapambano wakiwa na lengo la kujipanga upya ili kukabiliana na wapiganaji hao wa Boko Haram

Kwa mujibu wa jeshi la Cameroon, wanajeshi hao 500 wa Nigeria wamesafirishwa jumatatu wiki hii nchini Nigeria chini ya ulinzi mkali. Wanajeshi hao walitoroka mapigano yaliyokua yakiendeshwa na jeshi la Nigeria katika eneo la Banki dhidi ya Boko Haram, karibu na mpaka wa mji wa Mayo-Sava, nchini Cameroon ambako waliwasili wakiwa na silaha zao.

Baada ya kuwasili nchini Nigeria wanajeshi hao walipokelewa katika mji wa Maroua, na baadae walisafirishwa katika shule mbalimbali katika jimbo la Gazawa.

Mapigano kati ya jeshi la Nigeria na wapiganaji wa Boko Haram yameendelea, huku boko Haram ikichukua uamzi wa kuweka jimbo la Gwoza chini ya uongozi wa Khalifa, ambaye ni kiongozi mkuu wa kislam.