BURUNDI-Siasa

Burundi: Pierre Nkurunziza awonya baadhi ya wanasiasa

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza. REUTERS/Stringer

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, jumanne wiki hii, ametimiza miaka 4 tangu achaguliwe kuiongoza Burundi kwa muhula wa pili. Katika hotuba yake kwa taifa, Pierre Nkurunziza, amewataka wananchi kujiandaa kwa uchaguzi ujao na kuwatahadharisha wale wanaokusudia kupotosha uchaguzi huo.