SUDANI KUSINI-UN-Uchunguzi

Sudani Kusini: UN imeanzisha uchunguzi kuhusu ajali ya helikopta yake

Tổng thư ký Ban Ki-Moon trong cuộc họp báo ở trụ sở Liên Hiệp Quốc, New York, ngày 09/09/2013
Tổng thư ký Ban Ki-Moon trong cuộc họp báo ở trụ sở Liên Hiệp Quốc, New York, ngày 09/09/2013 REUTERS

Afisi za Umoja wa Mtaifa zilizoko Sudan Kusini zimeanzisha uchunguzi mkali kujua hasa kilichosababisha kuangushwa kwa  helikopta yao iliyokuwa  ikipaa kutoka  mji wa Wau, katika jimbo la Bahr El-Ghazal  Magharibi, kuelekea kwenye mji wa Bentiu katika jimbo  linalozalisha mafuta la Unity.Ni taarifa ya James Shimanyula

Matangazo ya kibiashara

Makao ya  afisi za  vikosi vya  kulinda amani  vya  Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, yamethibitisha kuwa helikopta yake aina ya MI-8 imewaua  wafanyakazi wake watatu na mmoja akanusurika baada ya kudondoshwa kutoka angani ilipokuwa ikielekea kwenye mji wa Bentiu katika jimbo lenye utajiri wa  mafuta la  Unity.

Kuangushwa kwa ndege hiyo kulisababisha vifo vya  wafanya kazi wa Umoja wa Mataifa ambao  ni wananchi wa Urusi, lakini mfanyakazi wa nne alinusurika na  kulazwa katika hospitali ya Bentiu ambako  anatibiwa
Kunusurika kwa mtu huyo mmoja kulithibitishwa na msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric.

“ Mmoja wa watu walionusurika amepewa matibabu na madaktrai wasio na mipaka katika mji wa Bentiu. Helikopta ilipoteza mawasiliano na Kitengo chetu”, amesema Dujarric.

Ingawaje Umoja wa Mataifa umeanzisha uchunguzi mkali kujua aliyehusika na kitendo hicho, tayari serikali ya Sudan Kusini kupitia msemaji wake rasmi wa kijeshi  kanali Philip Panyang Agwer, imedai  kuwa wapiganaji wanaomtii kiongozi wa waasi Riek Machar,  wanahusika na kuangushwa kwa helikopta hiyo.

“ Helikopta ilidondoka chini na kuwaua watu watatu kati ya wane waliokuwa ndani yake. Wote ni wageni. Mmoja wa waliokuwa ndani ambaye ni rubani wa ndege hiyo alinusurika.

Wanajeshi wa SPLA walimkimbiza rubani huyo aliyenusurika katika hospitali ya Bentiu kufanyiwa matibabu. Kwa sasa SPLA ndiyo inalinda helikopta kwenye eneo ilikodunguliwa” amesema Agwer.

Kwa upande wake, msemaji rasmi wa waasi Brigedia-Jenerali Lul Ruai Koang, amesema tuhuma za jeshi dhidi yao hazina msingi wowote.

“ Hiyo si kweli. Sisi hatuko sehemu  ilikoanguka helikopta. Hatuna vikosi eneo ilipodunguliwa helikopta . Eneo hilo linalindwa na vikosi vya serikali”, amesema Koang.

“ Vikosi vyetu havina uwezo wa kudondosha ndege. Hatuna kabisa uwezo wa kufanya hivyo” ameongeza Koang.