MAREKANI-SYRIA-IRAQ-ISIL-Usalama

Marekani: Barack Obama atafakari mbinu mpya ya kupambana na wapiganaji wa kiislam

Rais wa Marekani, BArack Obama, akibaini kwamba Marekani haijawa na mpango wa kuingia kijeshi nchini Syria dhidi ya wapiganaji wa makundi ya kiislam.
Rais wa Marekani, BArack Obama, akibaini kwamba Marekani haijawa na mpango wa kuingia kijeshi nchini Syria dhidi ya wapiganaji wa makundi ya kiislam. REUTERS/Larry Downing

Hali inaayojiri katika baadhi ya mataifa ya Mashariki ya Kati, hususan mapigano yanayoendelea nchini Syria na Iraq ni miongoni mwa masuala yanayoisumbua Marekani na washirika wake.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati ambapo wapiganaji wa makundi ya wanamgambo wa kiislam yameweka kwenye mtandao wao video inayoonesha namna wanavyo waua wanajeshi 160 wa Syria.

Rais wa Marekani, Barack Obama akieleza kuhusu hali hiyo inayajri nchini Syria, amesema hajawa tayari kuamuru jeshi lake kuanzisha mashambulizi ya anga katika maeneo yanayo shikiliwa na wapiganaji wa Kiislam, huku akibaini kwamba Marekani haiwezi peke yake kuanzisha operesheni hiyo, kuna ulazioma kueko na ushirikiano wa kimataifa, kutoka mataifa ya magharibi na ya kiarabu, amesema Barack Obama.

Barack Obama amebaini kwamba mashambulizi ya anga yanayoendeshwa na jeshi lake dhidi ya wapiganaji wa kiislam nchini Iraq, yameleta matunda, huku akimtaka rais wa Iraq kuunda serikali ya umoja itakayo shirikisha watu kutoka tabaka mbalimbali, wakiwemo watu kutoka jamii ya Wasuni. Hata hivo Barack Obama ametupilia mbali uwezekano wa kushirikiana na rais wa Syria, Bashar Al Assad kwa kupambana dhidi ya wapiganaji wa kiislam.

“ Tutaendelea kuunga mkono waasi wanaopinga utawala wa Bashar Al Assad, tunapaswa kuwapa nguvu waasi hao kwa kupambana na utwala wa Bashar Al Assad pamoja na wapiganaji wa kiislam wanaoshikilia baadhi ya maeneo nchini Syria. Mimi sioni mbinu gani Assad anaweza akatumia kwa nija moja au nyingine ya kurejesha amani katika eneo linalokaliwa na raia wengi kutoka Jamii ya Wasuni< amesema Assad.

Hayo yakijiri, wanajeshi 43 wa kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kutoka India wanaendelea kushikiliwa na kundi la watu wenye silaha katika milima ya Golan nchini Syria. Marekani imelituhumu tawi la Al Qaeda katika eneo hilo kuwashikilia wanajeshi hao. Wanajeshi wengine 75 wa kikosi cha Umoja wa Mataifa kutoka Ufilipino wamezingirwa na waasi wa Syria wanaopinga utawala wa Assad katika eneo hilo la Golan.