MALI-MNLA-Mazungumzo

Mazungumzo yanayojumuisha raia wa Mali yaanza kwa mara nyingine

Un tonneau peint aux couleurs du MNLA à la frontière du Mali et du Niger.
Un tonneau peint aux couleurs du MNLA à la frontière du Mali et du Niger. RFI/Moussa Kaka

Serikali ya Mali na makundi yenye silaha kaskazini mwa Mali wamekutana kwa mara nyingine tena jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa Algeria, Algiers, baada ya kuafikiana mwezi julai jinsi ya kuendeleza mazungumzo hayo. Mazungumzo hayo yanatazamiwa kuanza rasmi jumanne wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Sherehe za ufunguzi wa mazungumzo hayo yalichewa kwa muda wa saa mbili. Kwa mujibu wabaadhi ya wanadiplomasia, baadhi ya wajumbe wa makundi yenye silaha wamekua wamekataa kuingia katika ukumbi ulioandaliwa kufanyika mazungumzo hayo kutokana na utaratibu wa mapokezi, ambao wajumbe hao wamedai ulikua na mapungufu.

Hata hivo, baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya wajumbe hao na waziri wa mambo ya nje wa Algeria, wajumbe wa makundi ya MNLA, HCUA na MAA walikubali katika ukumbi huo kunakofanyika mazungumzo hayo, ambayo yanahudhuriwa na wawakilishi wa jumuiya ya kimataifa.

Kwa mujibu wa msemaji wa makundi hayo, Ould Ramadhan, hakuna haja ya kuweko na mvutano. “ Tumekua na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Algeria pamoja na baadhi ya wajumbe wa jumuiya ya kimataifa, kwa kutaka watuelekeze, amesema Ould Ramadhan, akibaini kwamba walikua wanataka wajuwe agenda ya mazungumzo.

Viongozi wa Mali wamebaini kwamba wamekuja kushiriki mazungumzo kwa nia nzuri, na wako tayari kuketi pamoja na makundi yote yenye silaha kwa lengo la kupatia suluhu tofauti zao. Hata hivo makundi yenye silaha bado yametofautiana kuhusu mazunguzo yaliyofanyika hivi karibuni.

Mmoja kati ya wajumbe hao aliyopea nafasi ya kuzungumza, amebaini kwamba mazungumzo ya awali yaligubikwa na kasoro nyingi, hususan “baadhi ya watu ambao wamekua kama wameyateka nyara mazunguzo hayo, huku wakiyafanya ya kwao”.

“Msipotezi nafasi hii, na nimeelewa chanzo cha kutofautiana kati yenu, kwa hiyo muweke kando tofauti zenu kwa masklahi ya taifa”, amesema waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Djibril Bassolé.

Viongoi wa Mali wamebaini kwamba kwa sasa hali inayojiri kwenye maeneo mbalimbali nchini Mali ni ya kuridhisha.

“ Hali inayojiri wakati huu ni ya kupongezwa, kwani hali ya utulivu imerejea, licha ya kuwa bado kuna machafuko yanayotokea katiak baadhi ya maeneo, lakini suala la usitishwaji mapigano katika eneo kulikokua kukiripotiwa mapigano, limetekelezwa na pande zote mbili”, amesema waziri wa mambo ya nje wa Mali, Abdoulaye Diop.