RWANDA-RCN-FDLR-Sheria-Siasa

Rwanda: wajumbe wa chama cha FPR watakiwa na rais Kagame kuwa na nidhamu

Tom Byabagamba (kushoto), mmoja wa wajumbe wakuu wa chama cha FPR anaezuiliwa kwa tuhuma za kuhatarisha usalama wa taifa, Agosti 29 mwaka 2014, akiwa na mwanasheria wake.
Tom Byabagamba (kushoto), mmoja wa wajumbe wakuu wa chama cha FPR anaezuiliwa kwa tuhuma za kuhatarisha usalama wa taifa, Agosti 29 mwaka 2014, akiwa na mwanasheria wake. AFP PHOTO/Stéphanie Aglietti

Rais wa Rwanda Paul Kagame amewataka wajumbe wa chama tawala FPR kuwa na nidhamu, wakati ambapo, baadhi ya maafisa wa jeshi kutoka chama hicho wamezuiliwa jela kwa tuhuma za kuchochea vurugu. Rais Kagame amewaonya wanajeshi wake katika mkutano wa bodi ya uongozi wa chama tawala.

Matangazo ya kibiashara

“Yeyote yule anaetafuta nafasi katika chama cha FPR, anapaswa kupitia chama, na iwapo utafikiria kupata nafasi nje ya chama cha FPR kupitia nje ya chama haitowezekana”, rais Paul Kagame amewaambia wajumbe 1500 kutoka chama hicho waliohudhuria mkutano huo jumapili mjini Kigali.

“ Huwezi ukatafuta nafasi katika chama wala wadhifa wowote katika uongozi wa nchi kwa kutetea mchango ulitoa kwa taifa hili miaka iliyopita”, ameongeza rais Kagame.

Kwa upande wake, mmoa kati ya wajumbe wa chama cha FPR, Oda Gasingizwa, amewaonya vikali baadhi ya wajumbe wa chama cha FPR, wakiwemo Rose Kabuye (mke wa David Kabuye anaezuiliwa) na Mary Baine (mke wa Tom Byabagamba anaezuiliwa pia).

“ Kuna wajumbe waliojihusisha na uhalifu dhidi ya Serikali (...), wakieneza uvumi, huku wakijiunga na makundi yasiyojulikana yenye lengo la kuhatarisha usalama wa taifa”, amesema Gasingizwa, huku akimnyooshea kidole balozi wa zamani wa Rwanda nchini Uholanzi, Immaculée Uwanyirigira.

“ Hatutokubali watu hao kuendelea kuwa m'bwa mwitu katika chama cha FPR, ameongeza Gasingiza.

Kwa upande wake mbunge kutoka chama cha FPR amekemea vikali kitendo cha mdogo wake, Odette cha kujiunga na chama cha upinzani kiliyoko ukimbizini cha RNC, ambacho serikali ya Kigali inadai kwamba ni kundi la kigaidi.

Akimalizia hotuba yake, rais Palu Kagame, amethibitisha kwa mara nyingine kwamba wajumbe hao, waliteuliwa na chama cha FPR, ili kuchukua nafasi walizo nazo wakati huu.