RWANDA-FDLR-Usalama, Siasa

Mpango wa kuwapokonya silaha waasi wa FDLR walaumiwa

Mpango wa kuwapokonya silaha waasi wa zamani wa Kihutu wa Rwanda walioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FDLR walalamikiwa kuzorota baada ya waasi hao kutowa masharti na visingizio.

Silaha za waasi wa Kihutu wa Rwanda katika msitu karibu na mji wa Pinga, kilomita 150 kaskazini magharibi na mji wa Goma, Februari mwaka 2009.
Silaha za waasi wa Kihutu wa Rwanda katika msitu karibu na mji wa Pinga, kilomita 150 kaskazini magharibi na mji wa Goma, Februari mwaka 2009. AFP PHOTO/ LIONEL HEALING
Matangazo ya kibiashara

Waasi wa FDLR wamemuandikia rais wa Zimbabwe na Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC Robert Gabriel Mugabe kwa madhumuni ya kupata fursa ya mazungumzo ya kitaifa baina ya serikali ya Kigali na wapinzani wote wakiwemo waasi wa FDLR.

Katika waraka huo, waasi hao wanajitambulisha kama wapiganaji kwa ajili ya uhuru, walinzi wa wakimbizi wa Rwanda, waathirika wa mauaji nchini Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yaliofanywa kulingana na wao na askari wa FPR wa Rwanda wakinukuu ripoti mbili za Jumuiya ya Kimataifa, yaani Gersony Report ya mwaka 1994 na Mapping report ya 2010.

Sehemu ya wapiganaji wa kundi la FDLR ambalo limesema wapiganaji wake wataendelea kujisalimisha
Sehemu ya wapiganaji wa kundi la FDLR ambalo limesema wapiganaji wake wataendelea kujisalimisha Reuters

hata hivyo, mjumbe maalum mpya wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Maziwa Makuu, Said Djinnit, akiendelea na ziara yake katika ukanda, amekutana na rais Paul Kagame wa Rwanda na waziri wa mambo ya Nje Louise Mushikiwabo na kuwathibitishia msimamo wa Umoja huo juu ya mpango wa kuwapokonya silaha waasi hao wa Kihutu wa Rwanda.

Kwa upande wake waziri Mushikiwabo, amesema serikali ya Rwanda inapatwa na mkanganyiko kufwatia makataa ya mwisho iliyopewa kwa waasi hao na kusema kuwa huenda upo mkono usioonekana ambao unataka kuwasafisha waasi hao badala ya kukomesha tishio.