MSUMBIJI-RENAMO-Siasa

Rais wa Msumbiji na kiongozi wa waasi wa Renamo wasaini mkaba wa kusitisha mapigano

Rais wa Msumbiji, Armando Guebuza, akiwa pamoja na kiongozi wa waasi wa Renamo, Afonso Dhlakama.
Rais wa Msumbiji, Armando Guebuza, akiwa pamoja na kiongozi wa waasi wa Renamo, Afonso Dhlakama. comunidademocambicana.blogspot.com

Rais wa Msumbiji Armando Guebuza pamoja na kiongozi wa waasi wa Renamo, Afonso Dhlakama wametia saini ijmuaa wiki hii kwenye mkataba wa amani.

Matangazo ya kibiashara

Mkata huo unasitisha machafuko yaliyodumu miaka miwili na kupelekea taifa hilo kuingia katika uchaguzi mwezi Oktoba.

Rais Guebuza na kuiongozi huyo wa waasi wa Renamo wametia saini kwene mkataba huo mbele ya zaidi ya wanadiplomasia 100 na viongozi mbalimbali serikalini walihudhuria sherehe hizo, ameshuhudia mwanahabari wa shirika la habari la Ufaransa AFP.

Kusaini wa kwa mkataba huo kunakuja baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya serikali ya Msumbiji na waasi kuafikiwa Agosti 24 mwaka 2014. Mara ya mwisho Afonso Dhlakama kukutana na rais wa Msumbiji Armango Guebuza ilikua mwaka 2011.

Kiongozi huyo wa waasi aliiwasili mjini Maputo alhamisi wiki hii akitokea uhamishoni.

Waasi wa Renamo walikua wakichukuliwa na serikali ya Msumbiji kama tishio kwa usalama wa taifa hilo, huku Renamo ikiituhumu serikali ya Maputo kuhusika na rushwa na kupora mali ya Taifa.

Mapigano yaliripotiwa kuwa makali kati ya jeshi na wapiganaji wa Renamo katika mwaka wa 2013, baada kuanzishwa kwa mazungumzo ambayo yalifeli na kupelekea Renamo kurudi msituni.