DR CONGO-Usalama

Mamia ya raia DR Congo kumzika Generali Lucien Bahuma

Generali Lucien Bahuma enzi za uhai wake alisimamia operesheni zilizofanikiwa kuwafurusha wapiganaji wa M23 na waasi wa Uganda ADF NALU
Generali Lucien Bahuma enzi za uhai wake alisimamia operesheni zilizofanikiwa kuwafurusha wapiganaji wa M23 na waasi wa Uganda ADF NALU desc-wondo.org

Aliyekuwa mkuu wa majeshi huko mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo generali Lucien Bahuma anatarajiwa kuzikwa leo huko mjini kisangani katika jimbo la mashariki.

Matangazo ya kibiashara

Generali Bahuma alifariki dunia mwishoni mwa mwezi Agost huko Afrika kusini baada ya kupatwa na maradhi ya kiharusi na baadaye kusafirishwa kwa dharura kutoka nchini Uganda alipokuwa katika mkutano wa viongozi wa kijeshi.

Generali Bahuma aliogoza oparesheni dhidi ya wapiganaji wa M23 huko mashariki mwa Congo na pia dhidi ya wapiganaji wa Uganda ADF NALU operesheni ambazo zilipata mafanikio makubwa.

Kifo hicho kinatokea ikiwa ni miezi nane baada ya kifo cha kanali Mamadou Ndala Mustapha,aliyekuwa kiongozi wa kijeshi katika eneo hilo aliyeuawa katika mazingira tatanishi na hivyo kuwafanya watu kutoamini kwamba jenerali Bahuma amefariki kutokana na maradhi,kama ilivyobainishwa na naibu mwenyekiti wa mashirika ya kiraia mashariki mwa Congo,Omar Kavota.