Raia watatu wa Italia wauawa nchini Burundi
Watawa watatu, raia wa Italia, wameuawa kikatili usiku wa jumapili kuamkia jumatatu wiki hii katika makaazi yao wilayani Kamenge katika manispa ya jiji la Bujumbura nchini Burundi, vyanzo vya utawala na polisi vimeeleza.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Kwa mujibu wa viongozi wa Italia, marehemu hao, Olga Raschietti, mwenye umri wa miaka 83 na Lucia Pulici, mwenye umri wa miaka 75, ni kutoka jamii ya wamisionari wa kanisa Katoliki, ambao makaazi yao ni wilayani Kamenge, kaskazini mashariki mwa mji wa Bujumbura. Maiti nyingine ya tatu imeokotwa mapema jumatatu alfajiri wiki hii kati ya saa tisa na saa kumi karibu na eneo walikouawa wenziye.
Watawa hao wamekua wakiishi katika eneo la kanisa Katoliki la parukiya ya Guido Maria Conforti. Kiongozi wa wilaya ya Kamenge Damien Baseka amebaini kwamba watawa hao wameuawa kikatili.
“ Mtuhumiwa ni kijana wa kiume, ambaye alionekana, akikimbia baada ya kutekeleza kitendo hicho kiovu saa kumi na moja jioni”, amesema Baseka.
Afisa mmoja wa polisi, ambaye hakupendelea jina lake litajwe, ameeleza kwamba watawa hao walikatwa vichwa, kabla ya mmoja wao kupigwa mawe usoni.
Kwa mujibu wa dayosisi ya Parma, nchini Italia, ambayo imerusha hewani picha za watawa hao wakivalia nguo za kawaida, nyuso zao zikiwa zimekunjika kutokana na uzee, wanadini hao wameuawa wakati wa jaribio la wizi lililokua likiendeshwa na kijana mmoja, bila hatahivo kutajwa jina lake.
Kwa mujibu wa afisa mmoja mwandamizi wa polisi nchini Burundi, kulingana na uchunguzi wa mwanzo, wizi huo si sababu ya kitendo hicho kivu.
" Mhalifu huyo hakuiba chochote hata pesa ziliyokua eneo la tukio hakubeba (...). Tumeanza kumtafuta muhusika, ambaye amejulikana, baada ya uchunguzi wetu”, ameseama afisa huyo wa polisi.
Mwezi Novemba mwaka 2011, mtawa raia wa Italia pamoja na raia wa Croatia waliuawa kwa risase wakiwa katika shughuli yao ya kidini katika mkoa wa Ngozi, kaskazini mwa Burundi. Vijana wawili walikamatwa, baada ya kutuhumiwa kuhusika na mauaji hayo. Vijana hao walihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kesi yao kuharakishwa.