Mjadala wa Wiki

Shirika la kutetea Haki za binadamu la Human Rights lawatuhumu wanajeshi wa AMISON kuhusika na Ubakaji nchini Somalia.

Imechapishwa:

Ripoti iliyotolewa na shirika la kimataifa la Human Rights Watch imewatuhumu askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika huko Somalia AMISOM, kuhusika na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, wanawarubuni wanawake kwa kuwapa chakula kama msaada ili wafanye nao ngono, tuhma ambazo AMISOM imekanusha.Kuzungumzia ripoti hii nimewaalika John Mwenda Mbijiwe ni mtaalamu wa masuala ya kiusalama akiwa Jijini Nairobi nchini Kenya, lakini pia Francis Auma ni mwanaharakati wa Haki za binadamu katika shirika linalotetea haki za Waislamu muhuri akiwa Mjini Mombasa pia nchini Kenya.

Studi RFI Kiswahili jijini Dar es Salaam
Studi RFI Kiswahili jijini Dar es Salaam RFI/BILALI