ARFIKA KUSINI-UFARANSA-RWANDA-Sheria

Afrika Kusini: Kayumba Nyamwasa atazamiwa kutoa ushahidi kuhusu kifo cha Habyarimana

Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa.
Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa. AFP/MARCO LONGARI

Nchi ya Afrika Kusini inafikiria hivi sasa ombi la mahakama ya Ufaransa ya kumsikiliza jenerali wa Rwanda Kayumba Nyamwasa, mmoja wa washukiwa tisa wanaohusishwa tangu mwaka 2006 katika kesi ya mashambulizi dhidi ya ndege ya Rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana.

Matangazo ya kibiashara

Jenerali huyo wa zamani wa jeshi la Rwanda na aliyekuwa mkuu wa kitengo cha intelijensia cha wapiganaji wa RPF katika miaka 1994 wakati wa shambulizi hilo ameomba tena hivi karibuni kusikilizwa kwa madai kwamba anao ushahidi tosha wa kuhusika kwa moja kwa moja kwa rais Paul kagame wa rwanda katika kutungua ndege ya rais habyarimana.

Kimsingi, majaji wa Ufaransa Trévidic na Poux wamehitimisha uchunguzi wao mapema mwezi Julai ikiwa ni mwanzo wa kipindi cha miezi mitatu ambapo majaji hao watahitahika kukusanya ushahidi wa ziada, dirisha la miezi mitatu ambalo litafikia mwisho wake mapema mwezi Oktoba.

Aidha, mwezi machi mwaka 2012, Kayumba Nyamwasa aliwahi kuomba kusikilizwa katika kesi hiyo na kutamka bayana kuwa kulinga na nafasi aliyokuwa nayo katika jeshi hilo anavyo vithibitisho tosha kuwa aliyekuwa mkuu wake wa zamani, Paul Kagame anahusika.

Tangu mwaka huo, maombi ya majaji hao wa Ufaransa hayajawahi kupatiwa ufumbuzi hadi hivi sasa ambapo serikali ya Pretoria inaangalia uwezekano wa kumsikiliza kayumba Nyamwasa katika ardhi ya Afrika kusini na si vinginevyo, hatua ambayo inakuja siku moja baada ya watuhumiwa wa jaribio la kumuuuwa jenerali huyo wameukumiwa miaka minane jela na Mahakama ya Afrika kusini.