AFRIKA KUSINI

Familia ya Reeva Steenkamp yasikitishwa na uamuzi wa Mahakama kuhusu Pistorius

Oscar Pistorius
Oscar Pistorius

Wazazi wa Reeva Steenkamp wanasema haki haikutendeka baada ya Mahakama Kuu mjini Pretoria nchini Afrika Kusini, kutompata na kosa mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius kumuua binti yao bila kukusudia.

Matangazo ya kibiashara

June na Barry Steenkamp wamesema wamesikitishwa na uamuzi wa Mahakama kuamini ushahidi wa Pistorius, na kuamua kuwa alitekeleza mauaji hayo bila kukusudia.

'Siwezi kuamini hata kidogo, Reeva hajapata haki, mimi nataka tu kufahamu ukweli," June Steenkamp alisema.

Siku ya Ijumaa, Jaji Thokozile Masipa alimpata na Pistorius na kosa la kuua bila kukusudia na kueleza kuwa hukumu ya kifungo chake itatolewa tarehe 13 mwezi ujao.

Kwa mujibu wa sheria za Afrika Kusini, Pistorius huenda akafungwa jela miaka 15 kwa kuua bila kukusudia au kutozwa faini.

Awali, Familia ya Pistorius ilieleza kuridhishwa kwao na uamuzi wa Mahakama wa kutompata Pistorius na kosa la mauaji kwa kukusudia kama ilivyokuwa inadaiwa na upande wa mashtaka.

Arnold Pistorius mjombake Pistorius amesema, “Sisi kama familia bado tunasumbuliwa na kilichotokea, tunaendelea kusitika na familia ya Reeva ambaye ahaezi kurejea tena duniani.

Ofisi ya kiongozi wa Mashtaka nayo imesema imesikitishwa na Mahakama kutompata na hati ya mauaji ya kusudia mwanaraidha huyo na inasubiri hukumu ya kifungo kabla ya kuamua ikiwa utakata rufaa au la.

Pistorius pia alipatikana na kosa la uzembe wa matumizi ya silaha alipokuwa Mkahawani jijini Johannerburg ambapo wakati akibadilishana silaha chini ya meza na rafiki zake, risasi ilitoka na kuharibu sakafu.