SIERRA LEONE-LKIBERIA-EBOLA-Afya

Sierra Leone: maambukizi ya Ebola yadhibitiwa

Serikali nchini Sierra Leone, inasema imefanikiwa pakubwa kudhibiti maambukizi mapya ya ugonjwa hatari wa Ebola baada ya amri ya siku tatu ya raia wa nchi hiyo kutotoka nje kumalizika saa sita usiku jana Jumapili.

Wafanyakazi wa idara ya afya wakibeba muili wa mtu aliefariki kutokana na Ebola, Septemba 11 mwaka 2014.
Wafanyakazi wa idara ya afya wakibeba muili wa mtu aliefariki kutokana na Ebola, Septemba 11 mwaka 2014. REUTERS/James Giahyue
Matangazo ya kibiashara

Sierra Leone ni mojawapo ya mataifa ya Afrika Magharibi ambayo yanakabiliwa na Ebola, na raia wake 550 wamepoteza maisha huku wengine wakifariki kutoka Liberia na Guinea.

Kwa kipindi hicho cha siku tatu, maafisa wa afya walizuru makaazi ya raia nchini humo na kutoa elimu ya namna ya kujizuia na maambukizi ya Ebola.
Shirika la afya duniani WHO linasema haya ndio maambukizi makubwa kuwahi kushuhudiwa duniani.

Muuguzi akimpa mwanamke alieambukizwa virusi vya Ebola  katika kituo maalumu kilichobobea katika maradhi ya maambukizi, mjini Kenema (Sierra Leone), Julai mwaka 2014.
Muuguzi akimpa mwanamke alieambukizwa virusi vya Ebola katika kituo maalumu kilichobobea katika maradhi ya maambukizi, mjini Kenema (Sierra Leone), Julai mwaka 2014. REUTERS/Jo Dunlop/UNICEF/Handout via Reuters

Mlipuku huo wa Homa ya Ebola umesababisha vifo vya watu 2600 katika nchi za Sierra Leone na Liberia tangu mwanzoni mwa mwaka 2014, na kusababisha mataifa hayo mataifa hayo kukabiliwa na mdororo wa kiafya ambao umeathiri sekta za jamii na uchumi.

Nchini Sierra Leone ambako Homa ya Ebola imewaua watu 562, raia milioni sita wa taifa hilo walitakiwa kubaki nyumbani kwa siku tatu mfululizo tangu ijumaa hadi jana jumapili. Operesheni hiyo imeendeshwa na watu 30,000 ambao walijitolea.

Watu 22 wamekutwa wameambukizwa virusi vya Ebola kufuatia operesheni hiyo ya siku tatu katika jimbo la magharibi, mji wa Freetown ikiwa ni moja ya sehemu ya jimbo hilo.

Naibu kiongozi wa idara ya afya, Saria Kamara, amesema watu kati ya 60 na 70 wamefanyiwa mazishi hivi karibuni kutokana na Homa aya Ebola.