UFARANSA-ALGERIA-Utekaji nyara

Algeria: raia wa Ufaransa atekwa nyara karibu na Tizi Ouzou

Video ya mateka wa Ufaransa anayeshikiliwa na kundi lenye mafungamano na IS iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii.
Video ya mateka wa Ufaransa anayeshikiliwa na kundi lenye mafungamano na IS iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii. Réseaux sociaux

Kundi lenye mafungamano na wapiganaji wa Dola la Kiislam limekiri jumanne wiki hii katika mkanda wa video, uliyothipitishwa na wizara ya mambo ya nje, kumteka nyara raia wa Ufaransa na limetishia kumuua ndani ya saa 24 iwapo Ufaransa haitasitisha mashambulizi yake dhidi ya IS nchini Iraq. 

Matangazo ya kibiashara

Mateka huyo, anashikiliwa na kundi la kijihadi la Algeria Jund Al Khalifa, “Wanajeshi wa Khalifa”, ambalo limetishia kumuua mateka huyo iwapo Ufransa itatekeleza mashambulizi mapya dhidi ya ngome za wapiganaji wa Dola la Kiislam nchini Iraq. Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imethibitisha kuwa mkanda huo wa video ni sahihi.

Video hiyo inayodumu kwa muda wa dakika nne, inaanza kwa ujumbe wa Abou Bakhr Al Baghdad akitolea wito wa kuua raia kutoka mataifa yanayosiriki katika muungano uliyoundwa kwa kupambana dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.

Katika muda wa dakika mbili, inaonekana picha ya raia wa Ufaransa anayeshikiliwa mateka akiika sakafuni akiwa amezunguukwa na watu wawili wenye silaha, huku wakiwa waficha nyuso zao na kitabaa cheusi. Baada ya ujumbe huo kwa lugha ya kiarabu, mateka huyo, akiwa amevaa miwani ameonekana akisoma ujumbe ambao ameuwasilisha kwa rais François Hollande.

Mateka huyo amesema anaitwa Hervé Gourdel, alizaliwa Septemba 12 mwaka 1959 mjini Nice. Amebaini kwamba aliwasili nchini Algeria Septemba 20. Amebaini pia kwamba anashikiliwa na kundi la watu wenye silaha linaloongozwa na Jund Al Khalifa, ambaye amemuomba rais wa Ufaransa kutoingilia kijeshi nchini Iraq.

Saa moja kabla ya video hiyo kurushwa hewani, wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilithibitisha kwamba kuna raia wa Ufaransa ambaye alitekwa nyara jumapili katika mji wa Kabylie.