UNSC-IS-Usalama

UN: azimio dhidi ya raia wa kigeni kujiunga na makundi ya kigaidi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lapitisha azimio dhidi ya raia wa kigeni kujiunga na makundi ya kigaidi.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lapitisha azimio dhidi ya raia wa kigeni kujiunga na makundi ya kigaidi. REUTERS/Adrees Latif

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana jumatano wiki hii na kuidhinisha azimio la kujaribu kuzuia watu kujiunga na makundi ya kigaidi yanayoendesha harakati zao Syria na Iraq.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo ulihudhuriwa na marais 28 kutoka mataifa mbalimbali. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeeleza kwamba watu hao wanaporejea katika mataifa yao wanakua kama tishio kwa usalama wa raia.

Azimio hilo limepitshwa kwa jumla ya wajumbe wa baraza hilo walioshiriki kikao. Azimio 2178 linaagiza serikali kuwazuia raia wao kujiunga na makundi ya kigaidi. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limezitaka serikali kupitisha sheria inayowaadhibu vikali watu wanaojiunga na makundi ya kigaidi.

Kwa mujibu wa Barack Obama, takribani wapiganaji 15,000 kutoka mataifa 80 wamejiunga miaka ya hivi karibuni na makundi ya kigaidi. Baada ya azimio hilo kupitishwa, rais wa Marekani ameonya: “ azimio hilo halitoshi linapaswa kuendana na vitendo”.

Marais wengi kutoka Afrika wamesema kwamba makundi mengi yanayo endesha harakati zao barani Afrika yamekua yakisajili watu kutoka mataifa ya kigeni.