Daktari Mkuu nchini Liberia ajitenga na watu baada ya naibu wake kufariki
Imechapishwa:
Daktari Mkuu nchini Liberia ameamua kujitenga na watu kwa siku 21 baada ya naibu wake kufariki kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola.
Naibu Waziri wa afya nchini humo Bernice Dahn, amethibitisha kujitenga na daktari huyo wa kike licha ya kutoonyesha dalili zozote za kuwa na Ebola.
Liberia inasalia nchi iliyoathiriwa mno na maambukizi ya Ebola miongoni mwa nchi za Afrika Magharibi na kulingana na takwimu za Shirika la afya duniani WHO, watu zaidi 1,800 wamepoteza maisha nchini Liberia pekee hadi sasa.
Nchi zingine zilizoathiriwa na Ebola ni pamoja na Guinea na Sierra Leone.
WHO imeonya kuwa ikiwa hali itaendelea kuwa hivi, watu zaidi ya elfu 20 wataambukiwa Ebola katika nchi hizo kufikia mwezi Novemba.
Marekani imetuma wanajeshi wake 3,000 nchini Liberia kusaidia kupambana na ugonjwa huo.