nchi za Jumuiya ya Semac zakutana kujadili kuhusu Ebola

kundi la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF wakitowa huduma kwa mshukiwa wa Ebola nchini DRCongo.
kundi la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF wakitowa huduma kwa mshukiwa wa Ebola nchini DRCongo. (Photo : Reuters)

Jumuiya ya kiuchumi na kifedha ya nchi za Afrika ya kati Cemac, imetowa mpango maalum kuhusu kupiga vita janga la Ebola. Walipokutana hivi karibuni jijini Congo-Brazzaville chini ya uongozi wa shirika linalo pambana na maradhi ya mlipuko katika ukanda wa Afrika ya kati, viongozi wa nchi sita wanachama wa Jumuiya ya Cemac wameamuru kuzidisha kasi za katika hatuwa za ulinzi dhidi ya maradhi hayo na mpango wa kukabiliana nayo iwapo yataibuka katika nchi wanachama.

Matangazo ya kibiashara

Nchi sita wanachama wa Cemac ambazo zipo katika hatari ya kukumbwa na maradhi ya Ebola yanayozikumba nchi za ukanda wa Afrika magharibi zinachukuwa hatuwa ya tahadhari iwapo maradhi hayo yatoibuka katika nchi moja mwanachama.

Kulingana na katibu mtendaji wa Cemac Roger Ayenengoye amesema hakuna nchi ambayo imeambukiwa na maradhi hayo, lakini hatuwa za tahadhari zinahitajika ili kujilinda na maradhi hayo. Nchi hizo ni pamoja na Congo Brazaville, Gabon, Cameroun, Equatorial Guinea, Jamhuri ya Afrika ya kati na Tchad.

Kuripotiwa kwa maradhi ya Ebola katika nchi ya Nigeria, jirani na Cameroun na Tchad pamoja na jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jirani ma jamhuir ya Afrika ya Kati na Congo-Brazzaville, imesababisha kuchukuliwa kwa hatuwa kadhaa katika baadhi ya mataifa wanachama za kuzuia mienendo ya nenda rudi kati ya wananchi.

Shirika la uakanda huo linalo husika na kupambana na maradhi ya mlipuko, linaona kuwa kuna haja ya kuzidisha kasi katika kuzidisha ulinzi zaidi na kupanga mipango madhubiti na ya dharura na nchi jirani katika kupiga vita maradhi hayo ya Ebola.

Mpango huo wa kukabiliana na Ebola utadumu kwa muda wa miezi sita na utagharamiwa na nchi sita wananchama.

Hayo yanajiri wakati huu naibu waziri wa afya nchini Liberia Bernice Dahn ambaye pia ni mkurugenzi wa idara za afya, amejiweka katika hali ya tahadhari ili kutowa mfano mwenyewe, kutokana na mmoja kati ya washirika wake kukumbwa na maradhi hayo. Naibu wake alifatiki siku ya alhamisi juma lililopita septemba 25. tangu kipindi hicho bibi Dahn ameamuwa kujiweka katika hali ya tahadhari pamoja na jopo la washirika wake kwa kipindi cha siku 21 kulingana na taratibu. Amesalia nyumbani kwake ambako anaendelea kufanyakazi na washirika wake.