RDCongo-sheria

Diomi Ndongala aiburuza serikali ya DRCongo katika Makama ya Kimataifa

Eugène Diomi Ndongala
Eugène Diomi Ndongala AFP PHOTO / JUNIOR D.KANNA

Mpinzani wa serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Eugene Diomi Ndongala ameifungulia mashtaka serikali ya rais Kabila kwenye kwenye mahakama ya kimataifa baada ya rufaa yake kugonga mwamba kwenye mahakama kuu nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Mwezi Machi uliopita, mahakama jijini Kinshasa ilimuhukumu kifungo cha miaka kumi jela kwa mokasa ya ubakaji dhidi ya binti mdogo, tukio ambalo kulingana na mahakama lilifanyika mwezi March iliopita.

Mbunge huyo wa zamani wa upinzani ameamuwa kuwasilisha mashtaka kwenye kitengo cha haki za binadamu cha Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi kwa kile alichosema kunyimwa haki ya kujitetea.

Kulingana na mawakili wake, lengo hasa la kuwasilisha mashtaka kwenye mahakama ya kimataifa ni kutaka uamuzi uliochukuliwa na mahakama ya jijini Kinshasa dhidi ya mteja wao, ubadilishwe kutokana na kuvunjwa kwa sheria.

Etienne Tshisekedi (Kati)  Eugène Diomi Ndongala (katika kanisa Notre-Dame de Kinshasa, Juni 22, 2012.
Etienne Tshisekedi (Kati) Eugène Diomi Ndongala (katika kanisa Notre-Dame de Kinshasa, Juni 22, 2012. AFP PHOTO / JUNIOR DIDI KANNAH

Majaji watano badala ya saba kama inavyoagiza sheria ndio waliomuhukumu mbunge huyo wa zamani wa upinzani, swala la kumyima haki ya kupewa matibabu, na kumzuia kukutana na watu wa familia yake kwa kipindi cha miezi mitatu, ni miongoni mwa mambo yanayogubikwa kesi ya kiongozi huyo ambapo mawakili wa Eugene Diomi Ndongala wanasema ni ukikukwaji dhahari wa haki za binadamu.

Jumla ni dosari 180 ndizo zilizokusanywa pamoja na kukabidhiwa kamati ya kimataifa ya haki za binadamu. Lengo hasa ni kutaka hukumu iliochukuliwa ya kifungo cha miaka kumi jela, kwa tuhuma za ubakaji wa msichana mdogo, ifutwe.

Matumaini ni kuona kwamba kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa inaamuwa kuhusu kesi hiyo ilioegemea upande mmoja. Kwa mujibu wa Georges Kapiamba, mwenyekiti wa shirika la haki za binadamu, anaona kwamba kulikuwa na uvunjifu wa haki, kwa hiyo, serikali inatakiwa kufuta uamuzi huo dhidi ya Diomi Ndongala na kumuacha huru na kumpa fidia.