SUDANI KUSINI - SHERIA

Amnesty International yahofia sheria tata kupasishwa nchini Sudani Kusini

wanajeshi wa Sudani Kusini mjini Juba
wanajeshi wa Sudani Kusini mjini Juba

Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International linatuhumu serikali ya Sudani Kusini hukusu pendekezo la sheria ya nchi iyo inayo towa uwezo zaidi kwa vyombo vya polisi kuwatia nguvuni washukiwa wa uhalifu katika nchi hiyo inayo kumbwa na mzozo wa kivita wa wenyewe kwa wenyewe.

Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo la haki za binadamu, linaona kwamba pendekezo hilo la sheria inayo towa uwezo zaidi kwa vikosi vya Usalama kuwatia nguvuni washukiwa wa uhalifu, kuendesha msaka, na kupora, litawanyima haki raia.

Pendekezo hilo liliandikwa tangu mwezi Mei, linapitia kwa mara ya tatu bungeni jumatano hii.

Idara ya Usalama ya NSS tayari inatuhumiwa na wananchi. Hivi karibuni idara hiyo ya usalama iliingia kati vyombo vya sheria na kuamuru kusitisha mjadala kuhusu njia za kumaliza mzozo wa kivita ulioanza tangu Desemba mwaka 2013, nchini humo.

Sudani Kusini inakumbwa na mzozo wa kivita ya wenyewe kwa wenyewe tangu kipindi hicho, mzozo ambao unashuhudiwa kutekelezwa mwa mauaji ya kikatili dhidi ya raia, na unaowapambanisha wannjeshi wa serikali na wale waasi tiifu kwa makam wa rais zamani Riek Machar.

Hakuna takwimu rasmi iliotolewa ya watu walipoteza maisha, inakisiwa kuwa watu maelfu ya watu walipoteza maisha katika vita hivyo huku watu wanaokadiriwa kugikia milio moja na laki nane wametoroka makwao.

Iwapo sheria hiyo itapasishwa bungeni, itawapa nafasi wajumbe wa NSS kuwakamata watu bila kuwa na waranti, na itawapa pia kinga ya kutofuatiliwa kisheria, hadi kupata amri ya wizara ya ulinzi.

Mtaalamu wa maswala ya sheria katika shrika la Amnesty International Elizabeth Deng, Sheria hiyo inaelezwa kuwa kinyume na katiba ya mpito iliopo nchi humo, lakini pia kinyume kabisa na sheria za kikanda na za kimataifa katika haki za binadamu